Nenda kwa yaliyomo

Joel Nanauka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dkt Joel Nanauka (alizaliwa Mtwara, 4 Julai 1983) ni mhamasishaji maarufu, mwandishi wa vitabu 45, na msomi aliyebobea katika masuala ya maendeleo na diplomasia ya uchumi.

Anajulikana kwa kazi yake ya utoaji mafunzo ya uongozi, mara nyingi akitoa hotuba na semina za kuhamasisha watu binafsi na mashirika kufikia malengo yao. Dkt Nanauka ameandika vitabu 45 na ni mzungumzaji maarufu kwenye matukio, akishiriki maarifa kuhusu mada kama vile mafanikio, uongozi, na ukuaji binafsi. Ana ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kama YouTube, Instagram, na Facebook, ambapo anashiriki maudhui ya kuhamasisha na kushirikiana na hadhira pana.[1]

Dkt Joel Nanauka alihitimu darasa la saba mwaka 1992, huku akishika nafasi ya 3 kimkoa kama mwanafunzi bora huko kwao mkoani Mtwara na hivyo kuchaguliwa kujiunga na shule ya vipaji Kibaha (Kibaha Secondary School) ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha sita.

Akiwa kidato cha pili 2000 alikuwa miongoni mwa wanafunzi bora 10 waliofanya vizuri katika kanda ya Mashariki

Mnamo mwaka 2002 kidato cha nne huku akiwa ni mwanafunzi bora kitaifa akipata ufaulu wa Alama A katika masomo tisa kati ya 10 aliyoyasoma na kufanikiwa kujiunga kidato cha sita hapohapo Kibaha Sekondari.

Alijiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2005 akisomea shahada ya Biashara na Uongozi na baadae alisoma Stashahada ya Juu ya Diplomasia Ya Uchumi (Post-graduate in Economic Diplomacy) na baadaye kupata Shahada ya Uzamili ya Maendeleo na Uhusiano wa Kimataifa (International Cooperation and Development).[2]

Mwaka 2024 Joel Nanauka alitunikiwa shahada ya heshima ya Uzamivu katika Uongozi na Usimamizi wa Biashara (PhD in Leadership and Business Management) na chuo kikuu cha Veridian kilichopo Atlanta,Georgia nchini Marekani.

Sky Joel Nanauka ni mme na baba wa watoto watatu wa kike. Mama yake anaitwa Anjela ambaye amewahi kuwa mwalimu mkuu wa shule ya Raha Leo huko Mtwara na baba yake ni mzee Nanauka.

Mafanikio

[hariri | hariri chanzo]

Licha ya kuwa miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa, Joel Nanauka amewahi kutajwa kuwa miongoni mwa vijana 100 wenye ushawishi zaidi barani Afrika, akibebwa zaidi na utoaji elimu kuhusu uchumi na uongozi katika majukwaa mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii na vitabu mbalimbali. Joel Nanauka amewahi kuajiliwa katika shirika la umoja wa kimataifa la Elimu , Sayansi na Utamaduni UNESCO.

Amewahi pia kutunikiwa tuzo ya I-Change Nations iliyotambua mchango wake wa kuleta mabadiliko kwa watu nchini Tanzania. Tuzo hizi zinatolewa na taasisi ya ICN iliyoko nchini Marekani.

Joel Nanauka ni mwanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali la Joel Nanauka Foundation lenye maono, lililojitolea kuboresha ubora wa maisha kwa watu wasio na fursa kupitia mipango endelevu, limejikita katika kutekeleza miradi inayoshughulikia mahitaji ya haraka ya jamii.[3]

  1. "Joel Nanauka katika Kinagaubaga na DW Kiswahili – DW – 03.05.2024". dw.com. Iliwekwa mnamo 2024-08-26.
  2. "Joel Nanauka – Life Coach. Author and Speaker" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-08-26.
  3. "Joel Nanauka Foundation". www.joelnanaukafoundation.or.tz. Iliwekwa mnamo 2024-08-26.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Joel Nanauka kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.