Joel Joseph

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mr Puaz
Mrpuaz.jpg
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Joel Vicent Joseph
Amezaliwa 31 Machi 1985 (1985-03-31) (umri 34)
Aina ya muziki Bongo Flava
Kazi yake Mwanamuziki,Mwandishi,Mwigizaji,
Miaka ya kazi 2002 mpaka Sasa
Studio Wasafi Records
Tovuti http://www.instagram.com/MrPuaz

Joel Vicent Joseph (alizaliwa tarehe 31 Machi 1985 jijini Arusha , Tanzania)[1] ni mwandishi,[2] , Mwigizaji[3][4] na Mwimbaji[1] kutoka Tanzania. Joel Joseph anakwenda kwa jina la kisanii liitwalo MR PUAZ[5][1] ambalo hulitumia kama mwanamuziki katika sanaa yake. Joel ni msimamizi[6] wa mwanamuziki kutoka Wasafi Records (WCB Wasafi) anayeitwa Harmonize.[7]

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Joel amezaliwa jijini Arusha , Tanzania tarehe 31 mwezi wa 3 mwaka 1985, mahali wazazi wake wamekulia na kuishi. Amehitimu masomo yake ya sekondari mwaka 2005 pale Marangu Sekondari na kuingia chuo cha cha ufundi wa Kompyuta kiitwacho New Horizon institute . Baadae aliendeleza masomo yake kwa kuchukua kozi mbalimbali kwa kutumia elimu ya mtandaoni (E-Learning) na kujichukulia vyeti vya kozi mbalimbali ikiwemo Career Management kutoka Harvards Business Publishing.

Uandishi[hariri | hariri chanzo]

Joel ameanza uandishi akiwa na umri wa miaka 26, Na hii ilitokana na kumiliki baadhi ya blogu zinazotoa makala mbali mbali za burudani, Amekuwa pia akiandika makala mbali kupitia media kubwa duniani kama Thrive Global, Tech Crates , Allbusiness na Marketing Insiders[8] .

Muziki[hariri | hariri chanzo]

Mr Puaz[9] ameanza muziki akiwa na miaka 21, alikuwa akijihusisha na kuimba nyimbo za wasanii wengine (Cover Songs) ambapo ilimpelekea kujua kwamba anauwezo wa kuimba hivyo kutunga nyimbo zake mwenyewe. Mwaka 2005 Mr Puaz aliingia kurekodi wimbo wake wa kwanza uitwao "SWEET BABY" iliyorekodiwa chini ya studio za Grandmaster Records zilizopo jijini Arusha,Tanzania.2006 alishiriki kutoa wimbo mwingine akiwa katika kundi akitumia jina Nizzo B. wimbo huo unaitwa "USIKU WA LEO" kazi ambayo imefanya vizuri kwenye Purebreak chart[10] kubwa za Ufaransa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 Mr Puaz Biography, Life Style and Profile - Howwe All Music. all.howwe.biz. Iliwekwa mnamo 2018-07-04.
  2. Joel Vicent Joseph | Thrive Global (en). www.thriveglobal.com. Iliwekwa mnamo 2018-07-04.
  3. Joel Vicent Joseph | Actor, Entrepreneur, Film Writer, — Bongo Movies - Buy Tanzania Movies and DVD's Online. www.bongocinema.com. Iliwekwa mnamo 2018-07-04.
  4. "Joel Vicent Joseph AKA Mr Puaz Returns to the Screens. - SmileCelebs", SmileCelebs (in en-US), 2018-03-03, retrieved 2018-07-04 
  5. Mr Puaz (en). Music In Africa. Iliwekwa mnamo 2018-07-04.
  6. Watiri, Sue, Meet the man tasked to handle Harmonize by Diamond (Photos) (in en-US), retrieved 2018-07-04 
  7. "ONE ON ONE: Harmonize", Daily Nation (in en-UK), retrieved 2018-07-04 
  8. "Avoiding Ghost Followers on Instagram", Marketing Insiders (in en-US), retrieved 2018-07-04 
  9. "Getting to know Joel Vicent Joseph alias “MR PUAZ” – Harmonize’s Manager", Campuslane (in en-US), 2018-06-05, retrieved 2018-07-04 
  10. Mr Puaz : tous les albums et les singles. www.chartsinfrance.net. Iliwekwa mnamo 2018-07-04.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]