Nenda kwa yaliyomo

Jiwe la Livingstone na Stanley

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jiwe la Livingston na Stanley ni jiwe lililowekwa mnamo Novemba 25, 1871 huko Mugere, kilomita kumi kusini mwa Bujumbura kwenye ukingo wa mashariki wa Ziwa Tanganyika.

Jiwe hilo lilihamishwa na kuwekwa mahali hapo ili kukumbuka kukutana kati ya mwanachuo David Livingstone na ripota kijana Henry Morton Stanley, aliyekwenda kumtafuta.

Mkutano huo ulifanyika siku chache mapema, Novemba 10, huko Ujiji, Tanzania ya leo. Mahali palipotajwa kwenye jiwe hilo ni mahali ambapo wavumbuzi hao wawili walitia nanga kuanzia Novemba 25 hadi 27, 1871.