Jin-Yi Cai
Jin-Yi Cai (alizaliwa 1961) ni mwanahisabati na mwanasayansi wa kompyuta wa Marekani mwenye asili ya China.[1] Yeye ni profesa wa sayansi ya kompyuta, na pia Profesa wa Steenbock wa Sayansi ya Hisabati katika Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison. Utafiti wake ni wa nadharia ya sayansi ya kompyuta, haswa nadharia ya ugumu wa hesabu.
Maisha ya Awali
[hariri | hariri chanzo]Cai alizaliwa huko Shanghai, Uchina. Alisomea hesabu katika Chuo Kikuu cha Fudan, na kuhitimu mwaka wa 1981. Alipata shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Temple mwaka 1983, shahada ya pili ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Cornell mwaka wa 1985, na Shahada ya tatu kutoka Cornell mnamo 1986, na Juris Hartmanis kama mshauri wake wa udaktari.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Two faculty members named Steenbock Professors". news.wisc.edu.
- ↑ "Curriculum vitae" (PDF). Iliwekwa mnamo 2021-09-12.
Makala haina vyanzo vya kutosha
Makala (au sehemu ifuatayo ya makala) inatoa habari bila kuonyesha vyanzo au uthibitisho wowote.
|
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |