Nenda kwa yaliyomo

Jimoh Buraimoh

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chifu Jimoh Buraimoh (akijulikana pia kama Jimoh Adetunji Buraimoh; alizaliwa 1943) ni mchoraji na msanii kutoka Nigeria.

Chief Buraimoh ni mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa walioibuka kutoka kwa warsha za miaka ya 1960 zilizoendeshwa na Ulli Beier na Georgina Beier huko Osogbo, jimbo la Osun, Nigeria. [1]

Maisha ya Awali na Elimu

[hariri | hariri chanzo]

Jimoh Buraimoh alizaliwa Osogbo, Osun State, Nigeria, mwaka 1943 katika familia ya kifalme ya Kiislam ya mji huo. Alishiriki katika warsha za miaka ya 1960 zilizoendeshwa na Ulli Beier, na pia alikuwa fundi mwanga katika tamthilia za Duro Ladipo.

Kazi za Jimoh Buraimoh zinachanganya mbinu za kisasa za Magharibi na mitindo ya Yoruba. Anatajwa kuwa mchoraji mkuu wa kwanza barani Africa alipobuni mnamo 1964 sanaa ya kisasa iliyochochewa na utamaduni wa Yoruba wa kuingiza miundo ya shanga kwenye nguo za sherehe na taji za shanga.[2] Mnamo 1972, aliiwakilisha Nigeria katika Maonesho ya Kwanza ya Biashara ya Waafrika wote yaliyofanyika Nairobi, Kenya. Moja ya michoro yake maarufu iliwasilishwa katika World Festival of Black Arts, Festac '77. Alikuwa Mnigeria wa kwanza kutunukiwa uanachama katika Chama cha Dunia cha Wasanii wa Mosaic wa Kisasa.

Jimoh Buraimoh pia ni msanii mwalimu mwenye ufanisi. Mnamo 1974, alifundisha katika Haystack Mountain School of Crafts huko Maine. Pia alifundisha katika Chuo Kikuu cha Bloomington na shule nyingine mjini New York, Boston na Los Angeles.

  1. "Chief Jimoh Buraimoh Organization". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-09-12. Iliwekwa mnamo 2014-07-29.
  2. "Chief Jimoh Buraimoh Organization". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-09-12. Iliwekwa mnamo 2014-07-29.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jimoh Buraimoh kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.