Jim Gray (mwanasheria)
James Polin Gray (alizaliwa Februari 14, 1945) ni mwanasheria na mwandishi kutoka nchini Marekani. Alikuwa hakimu msimamizi wa Mahakama ya Juu ya Kaunti ya Orange, California. Gray alikuwa makamu wa rais wa Chama cha Libertarian mwaka 2012, na pia mgombeaji wa chama hicho mnamo mwaka 2004 katika Seneti ya Marekani huko California.Ni mwandishi wa vitabu na pia muandishi wa tamthilia na ni mkosoaji mkubwa wa sheria za dawa za nchini marekani.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Gray ni Mzaliwa wa Washington, D.C. na alilelewa katika eneo la Los Angeles, huko California, Gray alipata digrii yake ya shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha California, Los Angeles mnamo mwaka 1966, kisha akafundisha katika Peace Corps huko Kosta Rika. Gray alirudi California na kupata digrii ya Udaktari wa sheria kutoka Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Southern California mnamo mwaka 1971.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jim Gray (mwanasheria) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |