Jennifer Maidman

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maidman akiitumbuiza moja kwa moja, 2013
Maidman akiitumbuiza moja kwa moja, 2013

Jennifer Maidman (zamani alijulikana kama Ian Maidman; alizaliwa 24 Januari 1958) ni mwanamuziki, mwimbaji, mtayarishaji, mtunzi wa nyimbo, mwigizaji na mwandishi wa nchini Uingereza ambaye ameshirikiana sana na vikundi na wasanii wengi wanaojulikana kimataifa.

Kazi yake inaonekana kwenye mamia ya rekodi tangu mwaka 1976 na kuendelea na amepokea tuzo nyingi, ikiwa ni pamoja na tuzo ya platinamu kutoka kwa British Phonographic Industry (BPI) kwa ajili ya albamu yake iliyojulikana kama "Hormonally Yours", ambapo alifanya kazi kama sehemu ya bendi ya "Dada Shakespears".

Alikuwa ni moja ya washiriki wakuu wa Penguin Cafe Orchestra kutoka mwaka 1984 hadi 2007.[1][2] Anajulikana zaidi kama mpiga gitaa la besi lakini pia huimba na kucheza, kibodi, ngoma, midundo, ukulele, cuatro na Chapman Stick. Mnamo Juni 2016 tovuti yake ilitangaza kwamba alikuwa akifanya kazi kwenye albamu ya solo huko Woodstock, New York akishirikiana na watu wengine wengine kama Jerry Marotta (ex Peter Gabriel), Annie Whitehead, na David Torn.[3] Albamu hiyo iliyojulikana kama "Dreamland" ilitolewa tarehe 1 Agosti 2017 na alishirikisha wasanii wengine kama Marotta, Torn na Whitehead, Tangu 2017 pia amekuwa akishirikiana mara kwa mara na shirika la sanaa la "New York The Secret [4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Penguin Cafe Orchestra – Songs, Playlists, Videos and Tours – BBC Music". Bbc.co.uk. Iliwekwa mnamo 21 October 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Penguin Cafe Orchestra Discography". Discogs.com. 18 December 2011. Iliwekwa mnamo 21 October 2015.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. "Jennifer Maidman". Jennifer Maidman. Iliwekwa mnamo 21 October 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. "Radio Kingston NY interview: Secret City Radio Hour: Jennifer Maidman". Iliwekwa mnamo 12 October 2019.  Check date values in: |accessdate= (help)