Jay Rosen
Mandhari
Jay Rosen | |
Amezaliwa | New York, Marekani |
---|---|
Kazi yake | Mwandishi, Profesa. |
Jay Rosen (amezaliwa Buffalo, New York, 5 Mei 1956) ni mwandishi na mwalimu wa uandishi wa habari katika Chuo Kikuu cha New York. Jay Rosen anajihusisha kwa karibu na masuala ya Uandishi wa Raia.
Kitabu chake kiitwacho What Are Journalists For? kilichotolewa mwaka 1996 kinazungumzia juu ya umuhimu wa kutumia zana mpya za habari kwa ajili ya mawasiliano na masikilizano.
Jay anaandika katika blogu yake iitwayo Pressthink ambayo inazungumzia juu ya taaluma ya uandishi katika zama za Intaneti. Pia huwa anaandika katika blogu ya The Huffington Post. Pressthink ilishinda tuzo ya Freedom Blog Award inayotolewa na shirika lisilo la kiserikali la Reporters Withouth Borders mwaka 2005.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Wasifu wa Jay Rosen Ilihifadhiwa 9 Mei 2007 kwenye Wayback Machine.
- Jay Rosen akihojiwa na Richard Poynder
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jay Rosen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |