Janice Lough
Janice Lough FAA ni mwanasayansi wa hali ya hewa katika Taasisi ya Australia ya Sayansi ya Bahari (AIMS) katika Chuo Kikuu cha James Cook,[1]anatafiti mabadiliko ya hali ya hewa, na athari za halijoto na kuongezeka kwa kaboni dioksidi kwenye miamba ya matumbawe. Alichaguliwa katika Chuo cha Sayansi cha Australia mwaka wa 2022 kwa ajili ya utafiti wake kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, miamba ya matumbawe, na kuendeleza historia ya hali ya juu ya mazingira na ukuaji kutoka kwa matumbawe, hasa Great Barrier Reef.[2][3]
Kazi yake
[hariri | hariri chanzo]Lough alipata shahada yake ya sayansi mwaka wa 1976, na shahada ya uzamivu mwaka wa 1981 katika Chuo Kikuu cha East Anglia, nchini Uingereza.[4]Alifanya kazi katika Chuo Kikuu cha Arizona, katika Maabara iitwayo Tree-Ring Research, kutoka mwaka 1982 hadi 1986, na baadaye akahamia Taasisi ya Australia ya Sayansi ya Bahari mwaka wa 1986.[5]
Lough ni mwanasayansi wa hali ya hewa ambaye amekuwa akifanya kazi juu ya ukuaji na rekodi za mazingira kutoka kwa matumbawe katika karne kadhaa zilizopita, na kuziweka katika muktadha wa kihistoria.[6]Pia anasoma jinsi mabadiliko ya hali ya hewa yameathiri mifumo ikolojia ya bahari ya kitropiki tayari, kwani ongezeko kubwa la joto ndani ya bahari ya kitropiki limerekodiwa. Anaripoti juu ya athari zinazothihirika na zinazoonekanazo za ongezeko hili la joto na matokeo yanayoonekana kwa miamba ya sasa.[7]
Taaluma ya Lough imejikita maeneo matatu, kuendeleza na kuchambua uundaji upya wa hali ya hewa ya paleo, kugundua asili, sababu na matokeo ya kutofautiana na kupishana kwa hali ya hewa kwenye miamba ya matumbawe ya kitropiki, pamoja na kuendeleza historia ya kufanya matumbwe yawe magumu kwa njia ya kukausha, kulingana na aina ya matumbawe hayo. Ana ujuzi katika ukuaji wa matumbawe, ukaushaji wa matumbwe, mabadiliko ya hali ya hewa na katika Great Barrier Reef.[2] She has expertise in coral growth, calcification, climate change and the Great Barrier Reef.[8]Pia, ni mwanachama wa ARC Center for Excellence for Coral Reef Studies, katika Chuo Kikuu cha James Cook.ref>"Janice Lough". STEM Women (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-26.</ref>
Kazi ya Lough imefafanuliwa na Carbon Brief,[9] ABC,[10][11] New York Times,na Australian Geographic,[12] pamoja na vyombo vingine vya habari[13] vikielezea athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa miamba ya matumbawe.[14]Pia amechapisha kwenye vyombo vya habari kuhusu kukauka kwa bahari.[15]
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]- 2020 – International Coral Reef Society (ICRS) Fellow award[16]
- 2022 – Fellow, Australian Academy of Science[3]
Baadhi ya machapisho yake
[hariri | hariri chanzo]- Lough, J.M.; Barnes, D.J. (2000). "Environmental controls on growth of the massive coral Porites". Journal of Experimental Marine Biology and Ecology. 245 (2): 225–243. doi:10.1016/S0022-0981(99)00168-9. PMID 10699212.
- Hobday, Alistair J.; Lough, Janice M. (2011). "Projected climate change in Australian marine and freshwater environments". Marine and Freshwater Research. 62 (9): 1000. doi:10.1071/MF10302. ISSN 1323-1650.
- Hughes, T. P.; Baird, A. H.; Bellwood, D. R.; Card, M.; Connolly, S. R.; Folke, C.; Grosberg, R.; Hoegh-Guldberg, O.; Jackson, J. B. C.; Kleypas, J.; Lough, J. M. (15 August 2003). "Climate Change, Human Impacts, and the Resilience of Coral Reefs". Science. 301 (5635): 929–933. Bibcode:2003Sci...301..929H. doi:10.1126/science.1085046. ISSN 0036-8075. PMID 12920289. S2CID 1521635.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Janice Lough – ARC Centre of Excellence for Coral Reef Studies". www.coralcoe.org.au. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-12-03. Iliwekwa mnamo 2022-05-26.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help) - ↑ 2.0 2.1 "Janice Lough". www.science.org.au (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-26.
- ↑ 3.0 3.1 "Academy announces 2022 Fellows for outstanding contributions to science". Australian Academy of Science (kwa Kiingereza). 2022-05-26. Iliwekwa mnamo 2022-05-26.
- ↑ "ORCID". orcid.org. Iliwekwa mnamo 2022-05-26.
- ↑ "Research Gate".
- ↑ "Townsville students submerged in marine science". Get Education (kwa American English). 2017-09-13. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-05-21. Iliwekwa mnamo 2022-05-26.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help) - ↑ sarah (2015-05-22). "Dr Janice Lough". Curious (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-26.
- ↑ "Janice Lough - Scimex". www.scimex.org. Iliwekwa mnamo 2022-05-26.
- ↑ "Ocean acidification: Decline of Great Barrier Reef likely to be worse than feared". Carbon Brief (kwa Kiingereza). 2016-02-23. Iliwekwa mnamo 2022-05-26.
- ↑ Monday, 30 May 2011 Anna SallehABC (2011-05-30). "Winners and losers in ocean acidification". www.abc.net.au (kwa Australian English). Iliwekwa mnamo 2022-05-26.
{{cite web}}
: CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ The Anthropocene: a new age of humans (kwa Australian English), Australian Broadcasting Corporation, 2016-11-15, iliwekwa mnamo 2022-05-26
- ↑ "More than 1000km of the Great Barrier Reef has bleached". Australian Geographic (kwa Australian English). 2016-04-08. Iliwekwa mnamo 2022-05-26.
- ↑ "Saving Our Marine Archives". Eos (kwa American English). 2017-02-24. Iliwekwa mnamo 2022-05-26.
- ↑ "A changing climate for coral reefs". Bulletin of the Atomic Scientists (kwa American English). 2016-10-11. Iliwekwa mnamo 2022-05-26.
- ↑ "Calcification in changing oceans". ScienceDaily (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-26.
- ↑ "Awards & Honors Recipients". International Coral Reef Society (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-05-26.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Janice Lough kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |