Nenda kwa yaliyomo

James F. Checchio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

James Francis Checchio (amezaliwa Camden, New Jersey, 21 Aprili 1966) ni askofu wa Marekani wa kanisa Katoliki.

Checchio alihudumu kama mkuu wa Chuo cha Kipapa cha Amerika Kaskazini huko Roma kutoka 2005 hadi 2016. Tarehe 8 Machi 2016, Papa Fransisko alimteua Checchio kuwa askofu wa Jimbo la Metuchen huko New Jersey.

James Checchio alizaliwa na James na Helen Checchio. Alihudhuria Shule ya St. John huko Collingwood, New Jersey, kisha Shule ya Upili ya Paul VI huko Haddon Township, New Jersey. Baada ya kuhitimu shule ya upili mwaka wa 1984, Cheechio aliingia Chuo Kikuu cha Scranton huko Scranton, Pennsylvania, ambapo alipata Shahada ya Sanaa katika falsafa mwaka wa 1988.[1]

  1. "Office of the Bishop - Most Rev. James F. Checchio, JCD, MBA". Diocese of Metuchen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-03-13.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.