Nenda kwa yaliyomo

Izimba Bhusu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Izimba Bhusu ni mojawapo ya majina ya kijiji cha Ussongo ambacho kinapatikana katika wilaya ya Igunga, mkoani Tabora. Kijiji hiki kwa upande wa magharibi kimepakana na kijiji cha Ndembezi, upande wa kaskazini kimepakana na Nyandekwa, kusini kimepakana na Ntigu ambapo kwa upande wa mashariki kimepakana na Moyofuke na Nanga.

Kijiji hiki kina historia ndefu kabla na baada ya ukoloni ambapo kiliwahi kuwa chini ya utawala wa watemi mbalimbali wa utemi wa Nyawa.

Pia kilikaliwa na wamisionari toka Ubelgiji na Italia. Kuna kanisa kubwa sana la Wamishenari wa Kikatoliki ambao walijenga na zahanati ya kwanza kabisa katika wilaya ya Igunga mnamo mwaka 1923 ambapo zahanati nyingine ilijengwa katika kijiji cha Nkinga na Wamishenari wa Kipentekoste mwaka 1936. Pia sekondari ya kwanza wilayani Igunga ilijengwa katika kijiji hiki mnamo mwaka 1952 ikijulikana kama St. Thomas Aquinas.

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tabora bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Izimba Bhusu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.