Ivoirité

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ivoirité (mara nyingine hutafsiriwa kwa Kiingereza kama Ivoirity) ni neno lilitumiwa kwa mara ya kwanza na Henri Konan Bédié mnamo mwaka 1995. Awali lilimaanisha utambulisho wa kitamaduni wa pamoja wa wote wanaoishi nchini Kodivaa, hasa wageni ambao ni theluthi moja ya idadi ya wakazi wote.

Wakati wa urais wa Henri Konan Bédié, neno hilo lilianza kutumika katika lugha ya kijamii na kisiasa ya nchi, na likatumika kama maelezo ya sifa za msingi zinazodaiwa za MKodivaa wa asili tofauti na wahamiaji.[1] Wakati wa urais wa Bedie, hali ya mvutano wa kikabila iliongezeka kwa kasi, na kulikuwa na mashambulizi yanayoongezeka dhidi ya wafanyakazi wa kigeni na pengo kubwa lililokuwepo kati ya eneo kuu la kaskazini lenye Waislamu wengi na eneo kuu la kusini lenye Wakristo wengi. Serikali yake ilijaribu kufafanua ni nani MKodivaa.

Kabla ya uchaguzi wa mwaka 1995 na 2000, sheria iliyopendekezwa na Henri Konan Bédié na kuthibitishwa na Mahakama Kuu ilihitaji wazazi wote wa Mgombea wa Urais wazaliwe ndani ya Kodivaa. Hii ilisababisha kumfungia nje Mgombea wa Urais wa kaskazini ' Alassane Ouattara, ambaye alidai kuwakilisha kaskazini, ambao kwa kawaida ni Waislamu, mara nyingi wafanyakazi maskini wahamiaji kutoka Mali na Burkina Faso wanaofanya kazi katika mashamba ya kahawa na kakao. Alassane Ouattara ambaye ni mwanachumi aliyefanya kazi na IMF, alikuwa waziri mkuu wa Kodivaa chini ya Rais Félix Houphouët-Boigny. Neno hili linahusishwa na Vita vya Pili vya wenyewe kwa wenyewe vya Kodivaa vilivyotokea mwaka 2010–2011, ambapo takriban raia 3,000 waliuawa.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Woods (2003) The Tragedy of the Cocoa Pod: Rent-Seeking, Land and Ethnic Conflict in Ivory Coast
  2. "Country Report on Human Rights Practices 2017 - Cote d'Ivoire". 20 April 2018.  Check date values in: |date= (help)
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ivoirité kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.