Ivica Zubac

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Zubac akiwa na timu ya Los Angeles Clippers 2022

Ivica Zubac (alizaliwa 18 Machi 1997) ni mchezaji wa mpira wa kikapu wa kikorasia anayechezea timu ya Los Angeles Clippers katika chama cha mpira wa kikapu cha kitaifa (NBA). Mwanzoni alichukuliwa na timu ya Los Angeles Lakers katika raundi ya pili ya drafti ya NBA mnamo mwaka 2016.[1]

Aliichezea Lakers hadi tarehe ya mwisho ya mkataba wake 2019, alipouzwa kwenda timu ya Clippers. Wakati wa mechi za mitoano za NBA 2021, aliisaidia Los Angeles Clippers kufikia fainali za michuano ya ukanda wa magharibi kwa mara ya kwanza katika historia ya timu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Lakers Draft Ivica Zubac with 32nd Overall Pick". www.nba.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-05-18.