Nenda kwa yaliyomo

Ivan Rakitic

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ivan Rakitic akichezea timu ya Sevilla.

Ivan Rakitic (alizaliwa 1988) ni mchezaji mtaalamu sana ambaye anacheza kama kiungo wa kati au mshambuliaji wa klabu iliyopo Hispania Barcelona FC na timu yake ya kitaifa Croatia.

Rakitić alianza kazi yake huko Basel na alitumia misimu miwili pamoja nao kabla ya kusainiwa na Schalke 04. Baada ya kutumia msimu mmoja na nusu Bundesliga, alisainiwa na Sevilla mwezi Januari 2011. Miaka miwili baadaye, Rakitić alikuwa nahodha wa klabu ya sevilla na alishinda magoli mengi katika msimu wake wa kwanza.

Juni 2014, Barcelona na Sevilla walikubaliana juu ya uhamisho wa Rakitić. Alifunga goli la kwanza la Mwisho wa Ligi ya Mabingwa 2015 na akawa mchezaji wa kwanza kushinda Ligi ya Mabingwa mwaka mmoja baada ya kushinda Europa League wakati akichezea vilabu viwili tofauti.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ivan Rakitic kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.