Nenda kwa yaliyomo

Ines Abdel-Dayem

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ines Abdel-Dayem

Ines Abdel-Dayem ni raia wa Misri na mpiga filimbi mashuhuri, apo awali alikua ni Mwenyekiti wa Cairo Opera House na ndiye Waziri wa Utamaduni wa Misri kwa sasa tangu Januari 2018.[1]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Ines Abdel-Dayem alisoma katika idara ya filimbi ya Cairo Conservatoire ambapo alihitimu mwaka wa 1984. Mnamo 1990, alipata diploma ya utendaji kutoka École Normale de Musique de Paris.[1][2]

Mnamo 2003, Abdel-Dayem aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa Cairo Symphony Orchestra. Mnamo 2005, alikua mkuu wa Conservatoire ya Cairo, na muda mfupi baadae akawa makamu wa rais wa Chuo cha Sanaa..[1] Mnamo Februari 2012, Ines Abdel-Dayem alikua mwenyekiti wa Cairo Opera House. Mnamo Mei 2013, alipoteza wadhifa huu baada ya Undugu wa Kiislamu kuingia madarakani nchini humo, lakini alirejeshwa muda mfupi baadaye Julai 2013.[1] Walakini, alikataa ofa ya kuwa Waziri wa Utamaduni wa nchi.[3] Egypte : une femme (presque) nommée ministre de la Culture,


Mnamo Januari 2018, aliteuliwa kuwa Waziri wa Utamaaduni wa Misri.[1] ndiye waziri wa pili wa Misri kutoka katika historia ya kisanii.[4] Mnamo Machi 2018, alimteua Mohamed Hefzy kama Rais wa mwaka wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Cairo.[5]

  • 2018: Tuzo ya Muziki wa Jazz ya Ujerumani[6]
  • 2001: Tuzo la Jimbo la Misri katika Sanaa[1]
  • 1982:
    • Tuzo ya nafasi ya kwanza katika Fédération Nationale des Unions des Conservatoires Municipaux[1]
    • Tuzo ya nafasi ya kwanza katika Concours Général de Musique et d'Art Dramatique[1]