Igowole

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Igowole ni jina la kata ya Wilaya ya Mufindi katika Mkoa wa Iringa, Tanzania yenye Postikodi namba 51409. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 13,459 waishio humo.[1]

Kuna maendeleo ya kasi sana na mji mdogo wa Igowole kwa sasa unatarajiwa kuwa makao makuu ya Wilaya ya Mufindi kusini zitakapogawanywa na Mafinga kubaki makao ya wilaya ya Mufindi Kaskazini.

Ni mji mwenye vivutio makampuni makubwa kama Unilever Tea Tanzania , viwanda kadhaa vya chai na mbao, mabwawa makubwa sana ya ngwazi, nzivi na kihanga. Mashamba makubwa ya chai yapo nje kidogo ya mji.

Msitu wa Saohill upo mwanzo wa mji hivyo mji upo kiutalii sana. Shughuli kuu za watu wa Igowole ni viwandani , biashara, kilimo, shughuli za mbao, na uvuvi katika mabwawa yaliyoyatajwa na pia ndiko viliko vyanzo vya mto Ruaha.

Mitaa ya mji mdogo wa Igowole ni Ligu, Ihanga, Mhamati, Kafufu, Nyuma ya Msitu, Mahaga, Mhemi, Nzivi, na Kisasa.

Marejeo

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Mufindi - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Bumilayinga | Idunda | Ifwagi | Igombavanu | Igowole | Ihalimba | Ihanu | Ihowanza | Ikweha | Isalavanu | Itandula | Kasanga | Kibengu | Kiyowela | Luhunga | Makungu | Malangali | Mapanda | Mbalamaziwa | Mdabulo | Mninga (Mufindi) | Mpanga Tazara | Mtambula | Mtwango | Nyololo | Rungemba | Sadani


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Igowole kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.