Nenda kwa yaliyomo

Idd el Fitr

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Msikiti wa Sultan Ahmed mjini Istanbul ikionyesha mapambo ya Ramadan kwa mwandiko unaong'aa "Penda na upendwe"

Idd el Fitr (Kiarabu: عيد الفطر ‘idu l-fiṭr; pia: Eid ul-Fitr, Id-Ul-Fitr, Iddul Fitri, Iddi al Fitr) ni sikukuu ya kiislamu inayomaliza mwezi wa Ramadan. Kipindi cha kufunga kinamalizika kwenye sikukuu hiyo. Ni sherehe ya siku tatu.

Idd el Fitr inaanza mara mwezi wa hilali umeonekana baada ya Ramadan.

Waislamu huvaa nguo safi mara nyingi nguo mpya na kutoa zawadi kwa maskini. Misikiti na nyumba mara nyingi zimepambwa. Ni nafasi ya kufurahia kati ya Waislamu.