Nenda kwa yaliyomo

Idd el Fitr

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Idd El Fitr)
Idd el Fitr
عِيدُ الْفِطْرِ
Msikiti wa Sultan Ahmed mjini Istanbul ukionyesha mapambo ya Ramadan kwa mwandiko unaong'aa "Penda na upendwe"
AinaSikukuu ya kidini, Uislamu
Pia huitwaEid al-Fitr, Iddi Ndogo, Sikukuu ya mfungo mosi
Maana / UmuhimuKusherehekea hitimisho la saumu ya Mwezi wa Ramadhani na kushukuru kwa kupewa nguvu za kutekeleza ibada hiyo
Tarehe1 Shawwal
Matendo makuuSala ya Eid, kutoa sadaka ya fitri (Zakat al-Fitr), kula asubuhi, kuvaa nguo mpya, na kutembelea jamaa
Inahusiana naRamadhani, Idd el Hajj

Idd el Fitr (Kiarabu: عيد الفطر ‘idu l-fiṭr; pia: Eid ul-Fitr, Id-Ul-Fitr, Iddul Fitri, Iddi al Fitr) ni sikukuu ya kiislamu inayomaliza mwezi wa Ramadan. Kipindi cha kufunga kinamalizika kwenye sikukuu hiyo. Ni sherehe ya siku tatu.

Idd el Fitr inaanza mara mwezi wa hilali umeonekana baada ya Ramadan.

Waislamu huvaa nguo safi mara nyingi nguo mpya na kutoa zawadi kwa maskini. Misikiti na nyumba mara nyingi zimepambwa. Ni nafasi ya kufurahia kati ya Waislamu.