Nenda kwa yaliyomo

I Am Frankie

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

I Am Frankie ni kipindi cha televisheni ambacho huonyeshwa kwenye chaneli ya Nickelodeon ambacho kinahusu mwanasayansi mmoja aitwaye Sigourney anayefanya kazi kwenye kampuni ya EGG (Electronic Giga Genetics) ambaye amemtengeneza androidi aitwaye Frankie. Lakini muongozaji wa kampuni aitwaye Kingston ataka kumtumia Frankie kwa ajili ya kampuni ya kijeshi iitwayo WARPA (Weaponized Android Research Project Agency) kwa ajili ya kazi maalumu baada ya Sigourney kujua hivyo anaacha kazi kwenye kampuni aliyokuwa anafanya kazi na kumchukua Frankie na kwenda kuishi naye na familia yake ambapo wanahama sehemu ambapo wanishi na kwenda kuishi mbali nakampuni ya EGG ili Frankie aweze kuishi maisha ya kawaida. Frankie anayazoea maisha yakuwa mwanafunzi wa shule ya Sepulveda High na anakuwa rafiki na msichana aitwaye Dayton na anapata mtu ambaye anaweka uadui na yeye aitwaye Tammy wakati familia yake ikijitahidi kuficha siri ILI kampuni ya EGG isiweze kumpata.Lakini Kingston anafanya kila awezalo ili ajue mahali ambapo Frankie anaishi ila siyo Kingston peke yake ambaye anamtafuta Frankie lakini na WARPA nayo ina mtafuta ila mwisho wa siku wanakuja kumkamata androidi mwingine aitwaye Andrew .Sasa Frankie anajaribu kila awezalo kumuokoa androidi mwenzake.

Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu I Am Frankie kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.