Nenda kwa yaliyomo

Ninga-bahari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Hydrobatidae)
Ninga-bahari
Ninga-bahari wa Wilson
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Procellariiformes (Ndege kama walinzi)
Ngazi za chini

Familia 2, jenasi 7:

Ninga-bahari ni ndege wa familia Hydrobatidae na Oceanitidae. Wana mnasaba na walinzi lakini ni wadogo kuliko hawa. Spishi za Hydrobatidae ni weusi au kijivucheusi na weupe kwa kiasi mbalimbali. Spishi za Oceanitidae ni weusi juu na weupe chini. Huruka kwa kupapatika. Hula gegereka wa planktoni na samaki wadogo wakiangama hewani na kukanyaga maji.

Kwa kawaida ninga-bahari huzaa kwa visiwa vya mbali visipokaa watu wala mamalia wengine. Huyatembelea makoloni yao usiku kuzuia ndege au wanyama mbua. Jike hulitaga yai moja tu kwa kawaida ndani ya kishimo au mwanya wa mwamba.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine

[hariri | hariri chanzo]