Husna Bai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Husna Jan au Husna Bai alikuwa mwimbaji wa muziki wa Thumri wa huko Banaras mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20. Alijulikana huko Uttar Pradesh kama mtaalamu wa khayal, thumri na tappa gayaki ambazo zote ni aina ya muziki. [1] Anasifiwa kwa kubadilisha tamaduni wa uimbaji mapema miaka ya 1900, kuimba nyimbo za kizalendo na kuwatia moyo waimbaji wengine kuiga mfano huo. Alifunzwa ama kufundishwa muziki na Thakur Prasad Mishra, na mchezaji maarufu wa Sarangi Pandit Shambunath Mishra, na tappa gayaki yake alipata ujuzi nayo chini ya ufundishaji wa Chote Ramdas Ji wa Banaras.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Bai aliishi katika kipindi kimja na Bhartendu Harishchandra, na aliwasiliana naye na kuchukua ushauri na maoni yake kuhusu semi za kishairi. Thumri yake na tanzu nyingine ndogo za thumri zilichapishwa kama Madhu Tarang (Sharma, 2012). Harishchandra pia alimfanya atunge Geet Govind akiwa na Jaidev. Alizingatiwa sawa na Vidyabari na Badi Moti Bai, mabingwa wa sanaa ya thumri na tappa. Bai alirejelewa kama 'Sarkar' au chifu, alipopanda hadi kiwango cha juu katika taaluma yake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "The Surprising Role Courtesans Played In Our Freedom Struggle". HuffPost India (kwa Kiingereza). 2019-07-27. Iliwekwa mnamo 2020-03-06.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Husna Bai kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.