Hospitali ya Kilutheri ya Haydom
Mandhari
(Elekezwa kutoka Hospitali ya kilutheri Haydom)
Hospitali ya Kilutheri ya Haydom (kifupi cha Kiingereza: HLH) ni hospitali iliyopo katika mji wa Haydom, magharibi mwa Mkoa wa Manyara.
Hospitali iko karibu km 300 kusini-magharibi kwa Arusha.
Hospitali ilianzishwa mnamo mwaka 1955 na wamisionari wa Kilutheri wa Norwei. Kwa sasa inamilikiwa na kuendeshwa na Dayosisi ya Mbulu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania