Hospitali ya Wasso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hospitali ya Wasso ni hospitali inayopatikana Loliondo, wilaya ya Ngorongoro katika mkoa wa Arusha.

Ilianzishwa kama hospitali ya Umisheni na hayati Dr. Herbert Watschinger kutoka Austria. Huyu alikuwa ni Padri na Daktari ambaye lengo lake kubwa halikuwa kuhubiri bali lilikuwa ni kujikita katika kutoa misaada mbalimbali kwenye jamii ambazo hazikupata huduma muhimu za kijamii. Ndipo alipofanikiwa kuanzisha Hospitali hii mwaka 1964. Aliamua kuanzisha hospitali hii ikiwa ni kuleta usawa, ubora, urahisi kwa jamii. [1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-12-04. Iliwekwa mnamo 2020-03-07.