Hospitali ya Mvumi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hospitali ya Mvumi ipo katika kijiji cha Mvumi, Mkoa wa Dodoma na ipo chini ya usimamizi wa kanisa la Anglikana Kanda ya kati mwa Tanzania. Hospitali hii hutoa huduma kwa wakazi wa Dodoma vijijini ikiwa na zaidi ya vitanda 280 za wagonjwa.

Hospitali ya Mvumi ni hospitali pekee Dodoma vijijini yenye uwezo wa kuhudumia zaidi ya watu 400,000 kwa mwaka. Mwaka 2008 kulitoka tamko la Raisi Jakaya Kikwete kwamba ingekuwa Hospitali ya Halmashauri na ikawa rasmi mwaka 2009. Serikali hulipa mishahara ya wafanyakazi wa hospitali na madawa tofauti na pesa za miradi na vifaa vya tiba.

Hospitali hii hupata msaada pia kutoka Uingereza (namba za usajili 289820). [1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-10-28. Iliwekwa mnamo 2020-03-07.