Nenda kwa yaliyomo

Hospitali ya Jakaya Kikwete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ni hospitali ya kitaifa ya umma iliyobobea katika utoaji wa huduma za matibabu ya moyo, mafunzo, na utafiti, iliyopo jijini Dar es Salaam, Tanzania. Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ilianzishwa mwezi Oktoba 2015 kupitia Waraka wa Uanzishwaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, 2015.[1] [2] Taasisi hii ipo ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika kata ya Upanga Magharibi, wilaya ya Ilala. Inahudumia wagonjwa wa watoto na watu wazima waliopewa rufaa ya kwenda kwenye hospitali iyo kutoka maeneo mbalimbali nchini. Huduma zinazotolewa ni pamoja na uchunguzi wa kitaalamu, upigaji picha za mwili, pamoja na taratibu za tiba ya moyo kupitia njia za upasuaji wa kifua na moyo.[3] Kuna mipango ya kupanua hospitali hii katika eneo la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili huko Mloganzila, nje kidogo ya jiji. Eneo hili jipya litakuwa na uwezo mkubwa zaidi kuliko lililopo sasa.

  1. JakayaKikweteCardiacInstitute|EAHealth. www.eahealth.org. Retrieved on 2024-10-09.
  2. "Hospital Overview — Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI)". www.jkci.or.tz. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-05-04. Iliwekwa mnamo 2020-03-10.
  3. "JK Cardiac Institute gets 300m/- donation to operate heart ailing kids". www.ippmedia.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-03-10.