Nenda kwa yaliyomo

Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hospitali ya Agha Khan, Dar es Salaam

Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam ni mojawapo ya huduma za afya za Aga Khan (AKHS) duniani. Ilianzishwa mwaka 1964 na kuanza kutoa huduma mbalimbali ikiwa na vitanda sabini na nne (74) vya kutolea huduma za kiafya kwa wagonjwa mbalimbali.[1]

Miaka ya hivi karibuni hospitali hii imekua kwa kasi kwa kutoa huduma bora kwa kutumia teknolojia na maabara za kisasa katika utoaji wa huduma zake. Lakini pia imepewa uwezo wa kuwa hospitali ya rufaa ambapo wagonjwa huandikiwa kuja kutoka hospitali zingine.[2] Vile vile hospitali ya Aga khan ya Dar es salaam inatoa huduma mbalimbali zikiwemo:Internal medicine (Kiingereza), Upasuaji (Kiingereza), Paediatrics (Kiingereza), Obstetrics (Kiingereza), Gynaecology (Kiingereza).[3]

Vifaa[hariri | hariri chanzo]

Huduma za hospitali hiyo ni pamoja na chumba cha wagonjwa mahututi chenye vitanda 15 kwa watu wazima, wagonjwa wa moyo na watoto, kitengo cha hemodialysis, kitengo cha matibabu ya moyo, vyumba vitano vya upasuaji, kitengo cha neurophysiology, wodi ya jumla ya taaluma ndogo zote, huduma ya radiolojia inayojumuisha MRI, CT na 3D mammografia na idara ya dharura 24/7.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Hospitali, chini ya mwavuli wa Chuo Kikuu cha Aga Khan inatoa programu za ukaaji katika Tiba ya Familia, Tiba ya Ndani na Upasuaji.

Uidhinishaji[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 2016, AKH ilipokea kibali cha Tume ya Pamoja ya Kimataifa (JCI), na kuifanya hospitali pekee iliyoidhinishwa na JCI nchini.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.