Hifadhi ya Taifa ya Manda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hifadhi ya Taifa ya Manda ni mbuga ya taifa ya nchini Chad .

Iko kusini mwa Chad karibu na mji wa Sarh na imepakana na Mto Chari upande wa mashariki na upande wa kusini magharibi ni barabara ya Sarh-Ndjamena.

Hifadhi hiyo inachukua zaidi ya hektari 113,000 na ilianzishwa mnamo 1965, kabla ya kuwa hifadhi ya wanyama tangu 1953.

Mamalia katika mbuga hiyo ni pamoja na simba na mamalia wengine wakubwa ambao wanaweza kuonekana tu wakati wa kiangazi.

Baadhi ya ndege wanaopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Manda Chad ni pamoja na Yellow penduline tit, Senegal Eremomela, blackcap babbler, white collared starling, bush petronia, Rufous Cisticola, Gambaga fly catcher na red faced pytilia miongoni mwa wengine wengi. [1] Hifadhi ya taifa ya Manda iliundwa awali kwa ajili ya ulinzi wa eneo la Derby, lakini kama tembo wa afrika, spishi hii ilitoweka kutoka kwenye hifadhi hiyo mwishoni mwa miaka ya 1980. [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Manda National Park Chad". Africa Tour Operators (kwa en-US). 2015-05-04. Iliwekwa mnamo 2020-12-17. 
  2. "The increasing pressure on natural resources around Manda National Park | West Africa". eros.usgs.gov. Iliwekwa mnamo 2020-12-17. 
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Manda kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.