Hemed Suleiman Abdalla

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hemed suleiman Abdulla

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
Aliingia ofisini 
2020
Rais Hussein Mwinyi
mtangulizi Seif Ali Iddi

tarehe ya kuzaliwa 5 Aprili 1973 (1973-04-05) (umri 51)
utaifa Mtanzania

Hemed Suleiman Abdulla (amezaliwa 5 Aprili 1973) ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika Serikali ya awamu ya nane iliyoingia madarakani mwaka 2020.[1] Anatokea katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Maisha yake[hariri | hariri chanzo]

Hemed Abdulla ni mzaliwa wa Kiwani Pemba, Jimbo la Mkoani.

Kazi yake[hariri | hariri chanzo]

Aliwahi kushika nafasi za uongozi akiwa Ofisa katika Wizara ya Fedha ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye ofisi zilizopo Pemba. Alipanda ngazi hadi kuwa Ofisa Mdhamini wa Wizara ya biashara na viwanda.

Mwaka 2015 alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Pemba na baada ya miaka miwili alipanda ngazi na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.

Mwaka 2020, Novemba Hemed Suleiman Abdulla aliapishwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi baada ya Dr. Hussein Mwinyi, Rais wa awamu ya nane wa Zanzibar kumteua kupitia nafasi kumi za Rais kwa mujibu wa Sheria. Novemba 9, 2020 akateuliwa kushika nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar akichukua nafasi ya Balozi Seif All Iddi aliyehudumu nafasi hiyo tangu Mwaka 2010 hadi 2020 na kustaafu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hemed Suleiman Abdalla kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.