Harakati ya Mazungumzo ya Kitaifa ya Tunisia
Wanne kwa Mazungumzo ya Kitaifa (ar. الرباعي التونسي للحوار الوطني, far. Quartet du dialogue national) ni maungano ya taasisi nne nchini Tunisia zilizounga mkono kujenga demokrasia na amani nchini baada ya mapinduzi ya mwaka 2011.
Baada ya mapinduzi hii na uchaguzi huru ya kwanza kulikuwa na kipindi cha mvurugo na mashambulio ya kigaidi kilichoelekea kuingiza Tunisia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe au udikteta mpya.
Katika hali hii taasisi nne ziliungana kwa shabaha ya kutunza demokratia na kuongoza mabadiliko kwa njia ya amani na haki. Taasisi hizi ni
- Chama cha Wafanyakazi wa Tunisia (UGTT, Union Générale Tunisienne du Travail)
- Umoja wa Makampuni ya Tasnia na Biashara ya Tunisia (UTICA, Union Tunisienne de l'Industrie, du Commerce et de l'Artisanat)
- Shirika ya Kutetea Haki za Binadamu Tunisia (LTDH, La Ligue Tunisienne pour la Défense des Droits de l'Homme)
- Umoja wa Wanasharia wa Tunisia (Ordre National des Avocats de Tunisie)
Harakati hii iliweza kukusanya wadau kutoka pande zote za siasa, uchumi na jamii kwenye mikutano ya majadiliano ya kitaifa.
Mwaka 2015 2015 harakati ya taasisi nne ilipewa Tuzo ya Nobel ya Amani kwa "michango muhimu katika ujenzi wa demokrasia ya kushirikisha pande zote nchini Tunisia baada ya mapinduzi ya 2011".
Kaci Kullmann Five, mwenyekiti wa kamati ya Nobel alsema: "Walileta mchakato ya kisiasa na ya amani wakati taifa lilikuwa karibu na vita ya wenyewe kwa wenyewe." [1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Luis Ramirez (2015-10-09). "Tunisian Mediators Win Nobel Prize". VOA.
Makala hii kuhusu mshindi wa Tuzo ya Nobel bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Harakati ya Mazungumzo ya Kitaifa ya Tunisia kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |