Nenda kwa yaliyomo

Graca Machel

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Graça Machel mwaka 2010

Graça Simbine Machel alikuwa mke wa marehemu Rais wa Msumbiji Samora Machel na tangu 1998 mke wa Nelson Mandela.

Alizaliwa tarehe 17 Oktoba 1946 nchini Msumbiji. Akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto sita wa mzee Simbine na bibi Nelly. Baba yake alifariki majuma matatu baada ya Graça kuzaliwa.

Graça alianza kujihusisha na siasa baada ya kwenda masomoni Lisbon, Ureno. Akiwa Lisbon alikutana na watu wengi wenye fikra za kimapinduzi waliokuwa wakijihusisha na harakati za ukombozi wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO. Serikali ya Msumbiji ilipopata taarifa za kujiunga kwake kwa siri na FRELIMO ilijiandaa kumtia jela mara tu atakaporudi nchini Msumbiji. Graça alipopata habari hizo alikimbilia nchini Uswisi. Mwaka 1973 akiwa bado Ulaya aliamua kujihusisha wazi wazi na harakati za ukombozi za FRELIMO. Chama cha FRELIMO kilikuwa na shule za sekondari katika nchi mbalimbali za Afrika zilizokuwa zikitoa elimu kwa wananchama wa chama hicho. Mwaka 1974 chama hicho kilimpeleka nchini Tanzania kuwa mwalimu wa shule ya sekondari ya FRELIMO iliyoko Bagamoyo.

Akiwa Tanzania alijifunza mafunzo ya kijeshi ya kujilinda na ni katika kipindi hiki ndipo alipoweza kukutana na Samora Machel ambaye baadaye alikuja kuwa mume wake na pia rais wa Msumbiji. Walifunga ndoa mwaka 1975 baada ya Msumbiji kupata uhuru wake toka kwa Wareno. Waliishi kama mume na mke hadi pale Samora Machel alipofariki kutokana na ajali ya ndege inayosadikiwa kuwa ilitunguliwa na makaburu wa Afika Kusini mwaka 1989. Kwa miaka mitano mfululizo tangu Samora Macheli afariki, Graça alivaa nguo nyeusi peke yake. Na ilipofika mwaka 1989 alistaafu wadhifa wake wa uwaziri na kujishughulisha na shughuli za maendeleo ya jamii hasa hasa watoto.

Mwaka 1998 Graça alifunga pingu za maisha kwa mara ya pili na rais wa kwanza wa Afrika Kusini huru, Nelson Mandela.

Maisha ya awali na Elimu

[hariri | hariri chanzo]
Graca na Samora Machel wakimkaribisha kiongozi wa Kikomunisti wa Kiromania Nicolae Ceauşescu, mjini Maputo, mwaka 1979

Graça Simbine alizaliwa siku 17 baada ya kifo cha baba yake, ni wa mwisho kati ya watoto sita,[1] katika kijiji cha Incadine, Mkoa wa Gaza, Afrika Mashariki ya Ureno ( Msumbiji ya kisasa). Alihudhuria shule za kimisionari za Methodisti kabla ya kupata ufadhili wa masomo katika Chuo Kikuu cha Lisbon nchini Ureno, ambapo alisoma Kijerumani na kwa mara ya kwanza akaanza kujihusisha na masuala ya uhuru.

Machel pia anazungumza Kifaransa, Kihispania, Kiitaliano, Kireno na Kiingereza, pamoja na lugha yake ya asili ya Xitsonga

  1. "Graca Machel: There Is Nothing Exceptional About Me..." This Day Live. 16 August 2014. Archived from the original on 13 July 2015.