Nenda kwa yaliyomo

Gordon Gray III

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gordon Gray III

Gordon Gray III (alizaliwa 1956) Ni profesa katika shule ya mahusiano ya kimataifa ya Penn. Alistaafu kama balozi wa masuala ya nje na pia alikua mshiriki wa zamani wa Huduma ya Mambo ya Nje ambaye pia alipata cheo cha waziri mshauri.alijiunga na kitivo cha chuo cha kitaifa mnamo Julai mwaka 2012 na alipewa wadhifa wa naibu kamanda na mshauri wa mambo ya nje ya kimataifa kutokea Juni 2014 hadi kufikia Juni 2015.Alikua balozi wa marekani nchini Tunisia na aliapishwa mnamo Agosti 20 2009 baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo na Rais Barack Obama, na kuhudumu hadi Julai 5, 2012.

Gordon Gray III alizaliwa katika Jiji la New York mwaka wa 1956. Alihudhuria Chuo Kikuu cha Yale, akipokea digrii yake katika Sayansi ya Siasa mwaka 1978. Gray baadaye alihudumu katika Peace Corps huko Oued Zem, Morocco hadi 1980. Kisha alihudhuria Chuo Kikuu cha Columbia, ambako alihitimu mwaka wa 1982 na Shahada ya Uzamili ya Mambo ya Kimataifa. Mnamo 2015, alipata tuzo ya heshima ya shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Ulinzi.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gordon Gray III kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.