Gisele Rabesahala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwanamke wa Kwanza Kiongozi wa Malagasy

Marie Gisèle Aimée Rabesahala (Antananarivo, Madagascar, 7 Mei 1929 – 27 Juni 2011)[1] alikuwa mwanamke wa kwanza mwenye nafasi ya Waziri katika serikali ya Madagascar.[2] Alijitolea maisha yake kwa uhuru wa nchi ya Madagascar na alitetea haki za binadamu. Alikufa tarehe ishirini na saba mwezi wa sita mwako wa 2011, siku moja baada ya maadhimisho ya miaka hamsini uhuru ya Madagascar. [1]

Maisha ya Utotoni[hariri | hariri chanzo]

Gisèle Rabesahala alipozaliwa, kisiwa cha Madagascar kilikuwa koloni la Ufaransa. Gisèle Rabesahala alitumia muda mwingi wa utoto wake nchini Ufaransa, Tunisia, na Mali kwa sababu baba yake alikuwa katika jeshi la Ufaransa.[3] Wakati baba yake alipokufa 1942, yeye na familia yake walirudi kisiwa cha Madagascar.[1] Alitamani kuwa mtawa wa kike na kujiona kama “mtetezi wa wasio na hatia.” [4] Ndoto hii ilimtia moyo wa kufuatilia elimu yake ambayo adimu ilikuwa wanawake wa Malagasy. Baadaye, ndoto yake ilibadilika na kuwa mwanasheria. Alipata shahada yake na akawa mpiga taipu kwa mahakama.[4]

Alipokuwa na umri wa miaka kumi na saba, akawa katibu wa Muungano wa Kidemokrasia wa Ukarabati wa Madagascar (MDRM).[3] MDRM ulikuwa muugano wa kisiasa uliyofanya kampeni za uhuru wa nchi.

Maasi Malagasy[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka wa 1947, wafuasi wa taifa la Malagasy walishambulia vituo vya kijeshi vya Ufaransa kwenye kisiwa. Kilichotokea ni jeshi la Ufaransa waliua wananchi wa Malagasy wengi.[1] Gisèle alifanya kampeni za kupigania haki za wafungwa wa kisiasa kutokana na maasi hayo. Alipambana kuwaweka huru maelfu ya wafungwa. Aliunga Kamati ya Umoja ya Madagascar ili kusaidia walioathirika.[3] Halafu alishiriki kuanzisha gazeti la “Imongo Vaovao” lililokuza mapigano ya uhuru wa Madagascar.[3] Alifanya kazi na wabunge ili kuomba haki kutoka kwa Rais wa Ufaransa.[1]

Kazi ya Siasa[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka wa 1956, Gisèle alikuwa mwanamke wa kwanza mteule kama diwani wa manispaa.[2] Halafu alianzisha uongozi chama cha siasa kilichoitwa ilimwito Muungano wa Watu wa Malagasy.[1][2] Alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza chama cha siasa Malagasy. Mnamo mwaka wa 1958, Gisèle aliunganisha mashirika matano ya kitaifa kuunda Chama cha Ubunge kwa Uhuru wa Madagascar (AKFM). [1] Mnamo mwaka wa 1960, Madagascar ilipata uhuru lakini Ufaransa ilifukuzwa mnamo mwaka wa 1976. Mnamo mwaka wa 1977, Gisèle alikuwa waziri wa kwanza mwanamke alipoteuliwa Waziri wa Utamaduni na Sanaa ya Mapinduzi. [3][5]

Uhifadhi wa Utamaduni na Urithi[hariri | hariri chanzo]

Alipokuwa Waziri, alijitahidi kuondoa athari za kikoloni na kufufua urithi wa Madagascar. [5] Alianzisha Maktaba ya Taifa ya Madagascar (1979) na aliunda Ofisi ya Haki ya Kunakili ya Malagasy (1985). [3] Ili kuhifadhi utamaduni, alihakikisha vitabu vya maktaba vimeandikwa na waandishi wa Malagasy na kuandikwa kwa Kimalagasy. [3] Alirejesha zaidi ya makaburi na maeneo ya kihistoria ishirini na tano.[2] Hadithia yake ya historia ya kisiasa ya Madagascar ilionyeshwa katika kitabu chake, “Uhuru uje Kwetu!” Alihudumu kama Waziri hadi mwaka wa 1991. [3]

Mauti[hariri | hariri chanzo]

Gisèle Rabesahala alifariki mnamo tarehe ishirini na saba mwezi wa sita mwaka wa 2011. Waandishi wa habari wa Madagascar walimtaja kama, “Mama Shujaa, mama wa taifa.”[1] Aliamini taifa heri ni lile limeundwa kutokana na urithi wake wa kitamaduni na kihistoria. [3] Alinukuliwa akisema mara moja, “Ikiwa hatujui tulikotoka, hatujui tuendako.” [3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 encyclopedia-womannica.simplecast.com https://encyclopedia-womannica.simplecast.com/episodes/leaders-gisele-rabesahala-z2ZHyWdK/transcript. Iliwekwa mnamo 2022-04-19.  Missing or empty |title= (help)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 "Gisèle Rabesahala". African Studies Centre Leiden (kwa Kiingereza). 2021-06-27. Iliwekwa mnamo 2022-04-19. 
  3. 3.00 3.01 3.02 3.03 3.04 3.05 3.06 3.07 3.08 3.09 Editorial Team (2018-11-09). "Gisèle Rabesahala: Visionary and A Human Rights Lawyer | African History". Think Africa (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2022-04-19. 
  4. 4.0 4.1 "Gisèle Rabesahala biography | Women". en.unesco.org. Iliwekwa mnamo 2022-04-19. 
  5. 5.0 5.1 Altius, Ave; Raveloharimisy, Joel (2016-07). "Women's Access to Political Leadership in Madagascar: The Value of History and Social Political Activism" (kwa English). ku. 132–142.  Check date values in: |date= (help)