Nenda kwa yaliyomo

Gareth Bale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gareth Bale akiwa na Real Madrid
Gareth Bale akiwa na timu yake ya taifa ya Wales

Gareth Frank Bale, (alizaliwa tarehe 16 Julai 1989 nchini Wales) ni mchezaji anayecheza nafasi ya winga katika klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Wales. Ana umaarufu wa kupiga mipira ya mbali, kupita katikati ya mabeki, na kasi kubwa na uwezo wake wa kutumia mguu wa kushoto na nguvu pia.

Alianza uchezaji wake kwenye klabu ya Southampton akicheza nafasi ya beki wa kushoto akiwa na umaarufu wa kupiga faulo, na baadaye kuhamishiwa klabu ya Tottenham Hotspur kwa ada ya £7 milioni, katika msimu wa 2009-10 chini ya Harry Redknapp alibadilishwa na kuwa winga na kuwa tegemezi kwenye timu na msimu wa 2010–11 aliiwezesha timu yake kufika UEFA Champions League na baadaye kuitwa mchezaji wa mwaka na timu ya mwaka ya UEFA.Na mwaka 2013 aliitwa mchezaji mdogo wa mwaka,Premier League mchezaji bora wa msimu, na kuwa mchezaji bora kwa tuzo za waandishi wa habari, na alikuwa mchezaji bora wa mwaka kwa mara tatu mfululizo.

Tarehe 1 Septemba 2013 aliuzwa Real Madrid kwa ada ya £ 90 milioni,na January 2016 vyombo vya habari vilisema uhamisho huo ulivunja rekodi ya dunia kwa kumpita Cristiano Ronaldo (£80) mwaka 2009. Akiwa Real Madrid alicheza sehemu kubwa na kuiwezesha kushinda 2013-14 Copa Del Rey, UEFA Champions League na kufunga kwenye mashindano hayo mawili. Alishinda UEFA Super cup na kuiwezesha timu yake kushiriki FIFA Club World Cup.

Miaka miwili baadaye alishinda UEFA Champions Leaguena kuibuka mchezaji bora wa msimu wa UEFA Champions League.Na aliibuka mshindi wa mchezaji bora wa UEFA.ESPN ilisema kuwa Bale alikuwa mchezaji bora wa kumi na mbili wa dunia.

Na ngazi ya timu ya taifa 2006 alikuwa mchezaji bora mwenye umri mdogo.Alifunga magoli 26 alikuwa mfungaji bora wa Wales na kuifikisha Wales kwenye UEFA Euro 2016.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gareth Bale kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.