Nenda kwa yaliyomo

Bamvua (mnyama)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Galigidae)
Bamvua
Bamvua wa wayo (Lepeophtheirus pectoralis)
Bamvua wa wayo (Lepeophtheirus pectoralis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Crustacea (Arthropoda wenye miguu yenye matawi mawili)
Ngeli: Maxillopoda (Crustacea wanaotumia maxilla kama miguu)
Nusungeli: Copepoda (Wanaogelea na maxilla zao)
Oda: Siphonostomatoida
Familia: Caligidae
Ngazi za chini

Jenasi 37; zile kubwa zaidi:

Bamvua ni gegereka wadogo wa familia Galigidae katika ngeli Maxillopoda. Kuna spishi 559 katika jenasi 37. Jenasi kubwa zaidi ni Caligus yenye spishi 268 na Lepeophtheirus yenye spishi 162. Bamvua ni vidusia wa nje ambao wanakula ute, tishu ya epidermi na damu za samaki wa bahari waliotumika kama mlisha. Vidusia hawa wanaweza kuwa shida kubwa katika ufugaji wa samaki, k.m. ule wa samoni katika bahari.