Nenda kwa yaliyomo

Gabriel Geay

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Gabriel Gerald Geay (alizaliwa Septemba 10, 1996) ni mwanariadha wa mbio ndefu kutoka Tanzania.[1] Geay ameshindana kwenye viwango vya juu kwenye umbali wa 5000 kupitia nusu marathoni[2].

Geay alishinda mbio maarufu za barabarani ikiwemo ya Peachtree Road race ya mwaka 2016[3] na Bolder Boulder 10,000 ya mwaka 2017 . Mpaka Julai 2018, Geay alikuwa amepata kiasi cha dola za kimarekani 33,000 kama hela ya ushindi[4].[5]

Mwaka 2017, alishiriki mbio za wanaume kwenye michuano IAAF World cross country mwaka 2017 iliyofanyika Kampala, Uganda.[6] Alimaliza nafasi ya 22.[6]

Mwaka 2019, alishiriki mbio za wanaume kwenye michuano ya IAAF World cross country yaliofanyika Aarhus, Denmark.[7] [8]Alimaliza nafasi ya 88.[8]

Mwaka 2021 alishika nafasi ya 6 akiweka rekodi mpya ya Tanzania ya 2:04:55 kwenye Milano Marathoni nchini Italia. Kwa rekodi hii ilimfanya afuzu kushiriki  michezo ya olimpiki 2020 kwenye marathoni ya wanaume jijini Tokyo. Alishiriki kwenye Olimpiki na mwenzake Alphonce Felix Simbu kwenye Marathoni ya wanaume mnamo August 2021.[9]

Mwaka 2023 alishika nafasi ya 2 akiweka rekodi mpya ya 2:06:04 kwenye Boston Marathoni nchini Marekani.[10]

Mashindano ya Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Jina la Mashindano Sehemu Nafasi Urefu wa mbio Muda aliotumia
2014 Michuano ya Vijana ya Afrika Addis Ababa, Ethiopia 4 5000 m 14:59.87
2017 Mashindano ya Dunia ya mbio ndefu Kampala, Uganda 22 29:47
2017 Mashindano ya Dunia Londoni, Uingereza 5000 m
2019 Mashindano ya Dunia ya mbio ndefu Aarhus, Denmark 87 2019 35:16
2019 Mashindano ya Afrika Rabat, Morocco 6 1500 m Mbio za mita 1500 Afrika kwa Wanaume 2019 3:39.29
2021 Mashindano ya Olimpiki 2020 Tokyo, Japani Mbio ndefu za Majira ya Joto 2020
2022 2022 Mashindano ya Dunia ya mbio ndefu Eugene, OR, Marekani 7 2022 Mashindano ya Dunia ya mbio ndefu Wanaume 2:07:31
2023 2023 Marathoni ya Bostoni, Marekani Bostoni, Marekani 2 Marathoni 2:06:04

Mataji ya Kitaifa

[hariri | hariri chanzo]
  • Ubingwa wa mbio za Marathoni Tanzania
    • 800 Mita: 2018
    • 1500 Mita: 2018
    • 5000 Mita: 2020
  1. "Gabriel Gerald GEAY | Profile | World Athletics". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-10-11.
  2. "ARRS - Runner: Gabriel Gerald Geay". arrs.auguszt.in. Iliwekwa mnamo 2021-10-11.
  3. "Unlikely winner of AJC Peachtree is Tanzanian Gabriel Geay". ajc (kwa English). Iliwekwa mnamo 2021-10-11.{{cite web}}: CS1 maint: unrecognized language (link)
  4. "ARRS - Runner: Gabriel Gerald Geay". arrs.auguszt.in. Iliwekwa mnamo 2021-10-11.
  5. "Gabriel Gerald GEAY | Profile | World Athletics". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-10-11.
  6. 6.0 6.1 0_R_COR (iaaf.org)
  7. "Gabriel Gerald GEAY | Profile | World Athletics". worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-10-11.
  8. 8.0 8.1 0_R_COR (iaaf.org)
  9. "Gabriel Gerald GEAY | Profile | World Athletics". worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-10-11.
  10. https://www.boston.com/sports/boston-marathon/2023/04/17/boston-marathon-2023-winners-results-list/