Nenda kwa yaliyomo

Fuzuli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Fuzulî)
Kwa eneo la utawala nchini Azerbaijan, angalia Fizuli.
Fuzûlî (1483?–1556)

Fuzuli (Kar./Kituruki فضولی) ilikuwa jina la kisanii la mshairi Muhammad bin Suleyman oğlu Füzuli (Kar. محمد بن سليمان) (takriban 14951556). Alikuwa mshairi mashuhuri wa Milki ya Osmani aliyeandika kwa lugha za Kituruki, Kiajemi na Kiarabu. Kituruki chake kilikuwa cha Kiazeri. Alikuwa pia mtaalamu wa hisabati na na falaki.

Fuzuli alizaliwa mnamo 1483 au 1495 katika eneo la Iraq ya leo ama mjini Najaf au Karbala. Familia yake ilitoka katika kabila ya Waturuki wahamiaji waliowahi kukaa mjini kwa vizazi kadhaa. Alipata elimu nzuri. Hakuna habari zaidi zenye uhakika juu ya maisha yake isipokuwa alikufa kutokana na ugonjwa wa kuambukizwa.

Mashairi yake yamehifadhiwa yakihesabiwa kati ya mifano bora ya mashairi ya Kituruki wa wakati wake. Aliandika mengi juu ya mapenzi lakini pia beti za kupinga makosa ya umma kwa mfano ufisafi:

سلام وردم رشوت دگلدر ديو آلمادىلر
Selâm verdim rüşvet değildir deyü almadılar.[1]
Nilisema "salaam" lakini hawakukubali kwa sababu haikuwa hongo.


Ukurasa kutoka mashairi yake Fuzuli


  1. Kudret 189

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]