Fura

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwanamke wa Kabila la Fulani akiandaa Fura
Mwanamke wa Kabila la Fulani akiandaa Fura

Fura ni aina ya chakula inayotoka kwa Fulanis na Hausas katika Afrika Magharibi[1]. Ni unga wa mtama, wenye "fura" ikimaanisha mtama. Pia huliwa nchini Niger na Ghana.[2] Mtama husagwa na kuwa unga, kukunjwa na kufinyangwa kuwa na umbo kama mpira, kisha kupondwa na kuchanganywa na Nono - maziwa yaliyochacha. Mchanganyiko wa fura na nono hutengeneza kinywaji cha Fura Da Nono, kinywaji kilichotengenezwa kienyeji ambacho kina wanga na nyuzinyuzi. Chakula cha fura na kinywaji cha fura da nono ni maarufu Kaskazini mwa Nigeria. Hutolewa wakati wa matukio maalum na kama chakula cha mchana.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Abdulkareem, U. D. (2019-10-24). Diary of A Peasant Child. ISBN 978-0-359-97353-8. 
  2. Relish The FULANI'S fura (en-GB) (2020-09-11).