Nenda kwa yaliyomo

Fred Msemwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fred Msemwa

Aliingia ofisini 
2014

tarehe ya kuzaliwa 14 Juni 1972 (1972-06-14) (umri 52)
Mbeya
utaifa Mtanzania
mhitimu wa Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
Chuo Kikuu cha Birmingham City,Uingereza
Fani yake Mhasibu wa Umma aliyeidhinishwa (Tanzania)
dini Ukristo

Fred Msemwa (alizaliwa 14 Juni 1972) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investment (WHI), kampuni iliyoanzishwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya uendelezaji wa milki na usimamizi wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja yenye makao yake makuu jijini Dodoma, Tanzania.

Ni mkaguzi wa hesabu, na mtaalam wa biashara, na mwandishi wa kitabu kiitwacho Usimamizi wa Biashara na Fedha[1]. Anajulikana kwa mchango wake katika kuendeleza upatikanaji wa nyumba za gharama nafuu, uongozi wa bodi za makampuni, uwezeshaji wa vijana na utetezi wa biashara ndogo ndogo nchini Tanzania.[2][3][4] [5]

Elimu na maisha yake ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Msemwa alizaliwa na kukulia katika Mkoa wa Mbeya uliopo kusini mwa Tanzania. Alisoma Shule ya Msingi Idweli na Mbeye One. Kisha alijiunga na Shule ya Sekondari ya Iyunga kwa masomo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne na baadaye katika Shule ya Sekondari ya vipaji maalumu ya Kibaha kwaajili ya Elimu ya Kidato cha Tano na Sita. Baada ya hapo alijiunga na kuhitimu Shahada ya Juu ya Uhasibu katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dar Es Salaam-Tanzania. Mwaka 1998 Msemwa alihitimu Shahada ya Juu ya Uhasibu(CPA) na kisha 2002, alihitimu Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Biashara MBA na kupata daraja la juu katika Chuo Kikuu cha Birmingham City, Uingereza. Ana Shahada ya Uzamivu ya Usimamizi wa Biashara kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na ni Mkurugenzi wa Bodi aliyethibitishwa na Taasisi ya Wakurugenzi ya Tanzania.[6]

Maisha ya kazi

[hariri | hariri chanzo]

Msemwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI)[7][8], kampuni ya uwekezaji nchini Tanzania inayohusika na uendelezaji milki na Usimamizi wa Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja. Alianza kazi yake ya uhasibu katika kampuni ya PUMA (wakati huo BP Tanzania) kisha akajiunga na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC); linalohusika na uendelezaji wa milki. Katika shirika la NHC alitoa mchango mkubwa katika kuiwezesha NHC kubadili na kutumia viwango vya kimataifa katika uandaaji wa taarifa za fedha. Akiwa na umri wa miaka 32 aliteuliwa kuwa Naibu Mkuu na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii nchini Tanzania. Wakati huo chuo kilizindua programu ya kwanza ya Diploma ya Usafiri na Utalii na kuanzisha kozi za ujasiriamali kwa wanafunzi wa utalii ili kuwapa uwezo wa kuanzisha na kuendesha biashara zao baada ya kuhitimu. Baadaye Msemwa aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Mamlaka ya Nishati na Maji (EWURA) ambapo alianzisha Idara ya Ukaguzi wa Ndani ya EWURA na akawa sehemu ya timu iliyofanikiwa kujenga EWURA kuwa mdhibiti wa maji na huduma anayeheshimika barani Afrika.[9] Akiwa WHI, Msemwa amehusika katika kuanzisha Mfuko wa Kwanza wa uwekezaji katika Milki (REIT) katika ukanda wa Afrika Mashariki ambao umejenga nyumba nyingi za gharama nafuu kwa ajili ya watumishi wa umma na waajiriwa wengine.[10][11] [12] Mnamo 2023, WHI ilizindua Mfuko mwingine unaoitwa FAIDA ambao ulipata mwitikio mkubwa wa asilimia 173% kutoka kwa wawekezaji.[13] Mfuko wa FAIDA umetajwa kuwa mojawapo ya mpango wa uwekezaji wa pamoja wa kidijitali Afrika Mashariki unaowawezesha wawekezaji wadogo wadogo wakiwemo wakulima, wachuuzi, wanafunzi na wafanyakazi wenye mtaji mdogo wa kuanzia shilingi elfu kumi za Tanzania kwa kutumia simu zao za mkononi bila kulazimika kujaza fomu za makaratasi. Mfuko huo umevutia wawekezaji wengi ambapo idadi yake inatajwa kuongezeka.

Msemwa aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzania[TAA][14][15] pia anajulikana kwa mchango wake katika bodi mbalimbali anazoendelea kuzitumikia ikiwemo Bodi ya CRDB Group[16][17][18] na ni mwenyekiti wa Bodi ya CRDB DR Congo.[19] Hapo awali aliwahi kuhudumu katika Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ya Tanzania na iliyokuwa benki ya TIB Corporate.[20]Bodi nyingine anazozitumikia ni pamoja na Bodi za Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Ukanda wa Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) na Bodi ya Shule za Agape.

Tuzo na kutambuliwa

[hariri | hariri chanzo]

Msemwa amewahi kupata tuzo na kutambuliwa katika jamii kutokana na taaluma yake na mchango wake katika kukuza biashara ndogo na eneo la uwezeshaji.[21] Amewahi kupokea tuzo ya Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) kutokana na mchango wake wa Kukuza ukuaji wa Biashara ndogo kupitia kampeni ya KUZA Biashara na pia amepokea Tuzo ya MAYODA kutokana na mchango wake katika ushauri wa vijana.Msemwa pia amewahi kupokea Tuzo ya Mkurugenzi Mtendaji Bora wa Mwaka wa Mashirika ya Umma ya Serikali 2022 kutoka kwa Tuzo za Kampuni Bora Afrika.[22][23]

  1. "Good business climate: A key to the success of any business". The Citizen (kwa Kiingereza). 2021-06-27. Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  2. "management – Watumishi Housing Investments" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  3. "The Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania". sagcot.co.tz. Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  4. "Watumishi wa umma washauriwa". Mwananchi (kwa Kiingereza). 2021-03-07. Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  5. "ACCOUNTANTS ANNUAL CONFERENCE PDF Free Download". docplayer.net. Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  6. "The Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania". sagcot.co.tz. Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  7. "Watumishi Housing Company (WHC) – AUHF" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  8. "Watumishi: VAT iondolewe kwenye nyumba". Mwananchi (kwa Kiingereza). 2021-03-10. Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  9. https://www.ewura.go.tz/wp-content/uploads/2019/06/Annual-Report-for-the-Year-Ended-30th-June-2011.pdf
  10. https://crdbbank.co.tz/storage/app/media/Our%20Investors/Annual%20Reports/CRDB-Group-and-Bank-Annual-Report-2021.pdf
  11. https://crdbbank.co.tz/storage/app/media/2022%20CRDB%20Annual%20Report.pdf
  12. "Nyumba 800 nafuu kujengwa Dar, Moro". Mwananchi (kwa Kiingereza). 2021-02-13. Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  13. "Faida Fund exceeds target, collects Sh12.9 billion". The Citizen (kwa Kiingereza). 2023-01-13. Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  14. "BoT yadai uchumi haupimwi kwa fedha za mfukoni". Mwananchi (kwa Kiingereza). 2021-03-03. Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  15. "Chama cha wahasibu chamkumbuka Dk Mengi". Mwananchi (kwa Kiingereza). 2021-02-18. Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  16. "Our Leadership". crdbbank.cd. Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  17. https://www.dse.co.tz/storage//securities/CRDB/news/JpSi2PzAhJFlVXSN9iZdU0k1qHt6zCmJ6kfup6ST.pdf
  18. https://crdbbank.co.tz/storage/app/media/Our%20Investors/Annual%20Reports/CRDB-Group-and-Bank-Annual-Report-2021.pdf
  19. "The Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania". sagcot.co.tz. Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  20. "Chama cha wahasibu chamkumbuka Dk Mengi". Mwananchi (kwa Kiingereza). 2021-02-18. Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  21. "Nouvelles – Page 19 – AUHF" (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  22. "Fred msemwa | Top 100 Executive List". top100executivelist.com. Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
  23. "More than 1000 houses for public servants to be constructed across the country this fiscal year". The Tanzania Times (kwa American English). 2023-08-12. Iliwekwa mnamo 2024-04-08.
Makala hii kuhusu mwanauchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fred Msemwa kama vile historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Pengine umewahi kuona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongezea habari zaidi.