Fortnite (mchezo wa video)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fortnite ni mchezo wa video ulioanzishwa na kampuni ya michezo ya video Epic Games mwaka 2017. Mchezo huu unahusu vita na umeweza kutwikwa taji kama Webby Awards, Teen Choice Awards na Game Critics Awards. Kuna vipengee viwili tofauti katika mchezo huu navyo ni

  • Fortnite: Save the World na
  • Fortnite: Battle Royale

Fortnite: Save the World[hariri | hariri chanzo]

Mchezo huu huhusu mchezaji akishirikiana na wachezaji wengine kupigana na vinyama (zombie) ambavyo vimekuja duniani baada ya dhoruba kupiga dunia na kuwaua viumbe wengi, takribani asilimia 98. Wachezaji wajaribu kuwaokoa walionusurika pamoja na kujaribu kutafuta data kuhusu kilichosababisha dhoruba ile.

Fortnite: Battle Royale[hariri | hariri chanzo]

Fornite Battle Royale yahusu mchezaji mmoja, wawili au wengi wakipigana katika vita. Wote wasafirishwa kwa ndege bila zana za vita hadi kwa kiwanja cha vita. Hapa wafaa watafute zana za vita na pia waibuke washindi huku wakijilinda kutokana na kuuliwa na wenzao.

Mapokezi na wachezaji wa michezo ya video[hariri | hariri chanzo]

Fortnite Save the World ilikuwa ilijipatia wachezaji milioni moja baada ya mwezi mmoja wa kuachiliwa. Battle Royale pia imekuwa ya kufana na kupendwa sana na wachezaji wa fortnite cheat

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Fortnite (mchezo wa video) kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.