Flowrence Jematiah Sergon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Flowrence Jematiah Sergon ni mwanasiasa wa Kenya. Tangu 2017 amekuwa mwanachama wa Bunge la Afrika Mashariki.[1]

Historia yake[hariri | hariri chanzo]

Flowrence Jematiah alisoma katika Shule ya Sekondari ya Marigat katika Kaunti ya Baringo, ambapo alikuwa mkuu wa wasichana katika shule hiyo. Kisha akasoma katika Chuo cha Mafunzo ya Tiba cha Kenya. Baadae akaingia katika siasa, alifanya kazi kupita Chama cha Republican na kisha kuwa mratibu wa kampeni za Chama cha Jubilee huko Baringo, Nakuru na Elgeyo-Marakwet.

Alichaguliwa na Chama cha Jubilee kwa Bunge la Afrika Mashariki, alichaguliwa kuwa mwanachama wa ELEA kwa kura 252. Yeye ndiye wa mwisho kati ya wawakilishi tisa wa Kenya kwa ELEA.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Kenya elects nine Eala MPs at last", 15 December 2017. 
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Flowrence Jematiah Sergon kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.