Femi Oke
Femi Oke | |
---|---|
Femi Oke (alizaliwa 1966) ni mtangazaji na mwandishi wa habari wa televisheni wa Uingereza. Femi alizaliwa nchini Uingereza na wazazi wenye asili ya Nigeria. Yeye ni msomi wa Chuo Kikuu cha Birmingham, ambako alipata shahada ya Bachelors katika maandiko ya Kiingereza na lugha. Sasa anaishi mjini New York na anaonekana kila siku kama mtangazaji na mhoijanaji katika kipindi cha redio cha The Takeaway katika kituo cha redio cha 'Public Radio International'.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Yeye ni mtangazaji wa zamani wa huduma ya hali ya anga ya CNN International katika mtandao wa kimataifa iliyo na makao makuu mjini Atlanta, Georgia. Alitangaza hali ya anga katika vipindi vya Your World Today na World News . Alitangaza pia kipindi cha Inside Afrika, kinachotangazwa na Isha Sesay, programu inayoangalia ndani ya uchumi, jamii na utamaduni na mwenendo wa mambo Barani Afrika.
Femi alianza kazi yake katika umri wa miaka 14 kufanya kazi kama mwandishi mdogo wa stesheni ya Uingereza ya kwanza ya majadiliano LBC. Katika mwaka 1993 Femi alikifanyia kazi kituo cha televisheni cha Wire TV, hii ilikuwa kabla ya kipindi cha Janet Street Porter cha L!VE TV. Femi alifanya kazi katika vipindi kadhaa katika kituo hicho, ikiwa ni pamoja na kipindi maarufu cha Soap on the Wire kilichoonyeshwa Jumamosi mchana, na mtaalam Chris Stacey. Mapema ya 1990, Femi alitangaza programu ya elimu ya sayansi ya kwanza ya Science In Action na pia alikuwa mtangazaji wa Top of the Pops. Pia alifanya kazi kwa GMTV, London Weekend Television, Men & Motors na Carlton Television. Alijiunga na CNN mwaka 1999, na kufanya kazi huko hadi 2008.
Amealikwa kufundisha kwa niaba ya World Meteorological Organization mjini Buenos Aires, Argentina, amefanya hotuba za mgeni katika Chuo Kikuu cha Emory Atlanta na amekuwa msemaji mgeni katika Umoja wa Kimataifa, kushughulikia Mpango wa Chakula Duniani mjini Roma, Italia.
Femi alionekana katika filamu fupi ya The Last Hour (2005).
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Wasifu wa CNN: Femi Oke Archived 6 Novemba 2008 at the Wayback Machine.
- Femi Oke: "Maisha yangu katika vyombo vya habari" Archived 1 Aprili 2008 at the Wayback Machine.
- Kipengo cha IMDb cha Femi Oke
- Takeaway juu ya PRI.ORG Archived 26 Februari 2010 at the Wayback Machine.
- Tovuti rasmi ya programu ya The Takeaway