Fatima Aziz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Fatema Aziz

Fatima Aziz (1973[1] - 12 Machi 2021) alikuwa daktari na mwanasiasa wa Afghanistan. Mnamo mwaka wa 2005, alichaguliwa kuingia kwenye bunge la Afganistan kama mwakilishi wa jimbo la Kunduz katika uchaguzi huru wa kwanza wa bunge wa miongo kadhaa nchini Afghanistan. Alichaguliwa tena katika uchaguzi wa 2010 na uchaguzi wa mwaka 2018.[2] Alihudumu kama mbunge hadi kifo chake kutokana na kansa mnamo mwaka 2021.[1]

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Fatima Aziz alizaliwa mnamo mwaka 1973 katika mkoa wa Kunduz, Afghanistan.[2] Mwaka 1987, alimaliza elimu yake ya sekondari katika Shule ya Upili ya Naswan mjini Kunduz. Alipata shahada ya udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Tiba cha Kabul mnamo mwaka 1993.[3]

Maisha Binafsi na Kifo[hariri | hariri chanzo]

Lugha ya kwanza ya Aziz ilikuwa Dari na pia alikuwa anazungumza lugha ya Pashto, Kiingereza, na Urdu.[3] Aliolewa na mwanaingine na alikuwa na binti wawili na wavulana wawili. Ndugu yake alikuwa mwakilishi katika Wizara ya Uchumi ya Kunduz.[2] Mwaka wa 2020, Aziz alipatikana na COVID-19, na aliweka video yake mtandaoni akiwa kitandani na bomba la oksijeni.[4] Alikufa kwa kansa mnamo tarehe 12 Machi 2021, katika hospitali nchini Uswisi.[1][2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 "Fatima Aziz 'member of parliament' dies of cancer at 47", Khaama Press, 12 Machi 2021. 
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 "Database". Afghan Bios. Iliwekwa mnamo 23 Septemba 2019. 
  3. 3.0 3.1 "Wolesia Jirga (Bunge la Watu): Wasifu wa Fatima Aziz". Bunge la Kitaifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Afghanistan. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-05-02. Iliwekwa mnamo 14 Machi 2021. 
  4. Tameem Akhgar (2 Julai 2020). "Long-Shut Factory Helps COVID-Struck Afghans Breathe Free". The Diplomat. Iliwekwa mnamo 12 Machi 2021. 
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fatima Aziz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.