Nenda kwa yaliyomo

Mafarisayo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Farisayo)
Sanamu za udongo za Mafarisayo zilizotengenezwa na Giovanni d'Enrico huko Varallo (Italia).

Mafarisayo waliunda madhehebu mojawapo ya Uyahudi ambayo wakati wa Yesu Kristo iliweza kufikia 5% ya Wayahudi wote, lakini ilikuwa na athari kubwa katika jamii yao, kutokana na sifa ya kuwa wanadini hasa. Jina lenyewe lina maana ya waliojitenga (na wakosefu) ili kushika kiaminifu masharti yote ya Torati ya Musa.

Mafarisayo wanajulikana hasa kutokana na Injili ambazo zinawataja kwa kawaida kama wapinzani wa Yesu, ingawa yeye alikuwa anakubaliana nao katika mafundisho mengi ya imani tofauti na yale ya Masadukayo, dhehebu jingine kubwa lililokuwa na wafuasi hasa kati ya makuhani.

Mafarisayo walianza mwishoni mwa karne ya 2 K.K. na kuendelea kustawi hadi mwaka 70 B.K., wakati Yerusalemu ilipoteketezwa na Warumi. Maangamizi ya hekalu yalivunja nguvu ya Masadukayo na kuwaachia Mafarisayo uongozi wa dini yao.

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mafarisayo kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.