Fadi Ghandour
Fadi Ghandour | |
---|---|
Makazi | Dubai, United Arab Emirates and Amman, Jordan |
Fadi Ali Ghandour (1959) ni mjasiriamali mwenye asili ya Kijordania, ambaye anafahamika zaidi kama mwanzalishi na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya usafirishaji ya Aramex, ambayo hujihusisha na maswala ya usafirishaji wa mizigo mbalimbali duniani. Ghandour alihusika katika uanzishwaji wa Aramex mwaka 1982[1] huko Amman, Jordan na amekuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo tangu wakati huo. Aramex ndio kampuni ya kwanza ya kiarabu kujisajili katika soko la hisa la NASDAQ.
Halikadhalika, Ghandour ni mwanzilishi mshiriki wa tovuti ya Maktoob.com, ambayo ndio mtandao mkubwa zaidi ya watu wa jamii ya waarabu duniani. Mtandao wa Maktoob ilichukuliwa na Yahoo! mwaka 2010. Ghandour pia ni mwanachama wa bodi ya Abraaj Capital ambayo ni moja ya makampuni makubwa zaidi katika ukanda wa Mashariki ya kati na Asia ya kusini. Pia ni moja kati ya waanzilishi wa Endeavor, iliyopo Jordan, na pia anashiriki kama mshauri katika kamati ya shule ya biashara ya Suliman S, Olayan School of Business iliyopo katika chuo kikuu cha Beirut. Kati ya mwaka 2003 na 2005, alikuwa mwenyekiti wa taasisi ya Young Presidents' Organization kwa upande wa Mashariki ya kati na Afrika ya kaskazini.
Gandour ana shauku ya kusaidia na kukuza wajasiriamali wadogo wadogo hasa katika jamii ya waarabu na pia amekuwa akiwekeza katika miradi mbalimbali ya kijasiriamali iliyopo Mashariki ya kati na Afrika ya kaskazini. Pamoja na mambo mengine, pia ni mwanzilishi wa mtandao wa Ruwwad for Development Archived 7 Januari 2014 at the Wayback Machine., ambao ni mtandao wa kijamii wenye lengo la kuinua jamii iliyo ukingoni kwa kutumia harakati mbalimbali za kijamii na kielimu. Pia ni moja kati ya wanakamati katika bodi ya benki ya National Microfinance Bank ya Jordan.
Pia amefanya kazi kama makamu mwenyekiti wa bodi ya Jordan River Foundation kwa takribani miaka 10
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Encyclopedia.jrank.org & CNN Interview