Ethanoli
Ethanoli (pia: alkoholi ethili) ni dawa lililopo ndani ya aina zote za vinywaji vya pombe.
Kikemia ni kampaundi ogania inayopatikana kama kiowevu kisicho na rangi. Ikiwa ni dawa safi inawaka haraka lakini mara nyingi hupatikana kama mchanganyiko pamoja na maji katika aina za pombe; hapa inawaka tu kama asilimia yake inapita kiwago cha 60%.
Fomula yake ni C2H5OH inayoandikwa pia C2H6O. Ni dawa lenye tabia ya sumu kiasi kwa mwili wa kibinadamu pia ina tabia ya kuyeyusha.
Ethanoli kama fueli
[hariri | hariri chanzo]Ethanoli ina pia matumzi ya fueli badala ya petroli. Inawaka ndani ya injini ama peke yake au ndani ya mchanganyiko wa petroli na ethanoli.
Nchini Brazil ethanoli hutengenezwa kwa wingi kutokana na miwa na sasa inatosheleza asilimia 18 ya mahitaji ya fueli ya magari katika nchi hii. [1] Watu wengine wanaona tatizo katika teknolojia hii maana mashamba makubwa yanatumiwa kwa miwa hayapatiokani tena kwa vyakula na maeneo makubwa ya misitu asilia yametumiwa pia..
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "America and Brazil Intersect on Ethanol". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-26. Iliwekwa mnamo 2010-08-22.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- E85 is an alcohol fuel mixture: 85% ethanol + 15% gasoline - US E85 refueling map Ilihifadhiwa 21 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- International Chemical Safety Card 0044
- Molview from bluerhinos.co.uk Ilihifadhiwa 25 Septemba 2008 kwenye Wayback Machine. See Ethanol in 3D (may take over a minute to load using a dial-up connection)
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ethanoli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |