Ethan Ampadu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ethan Ampadu

Ethan Ampadu (alizaliwa 14 Septemba 2000) ni mchezaji wa soka ambaye anacheza kama kiungo wa kati au kiungo mkabaji wa klabu ya Chelsea ya Ligi Kuu ya Uingereza na timu ya taifa ya Wales.

Kazi ya klabu[hariri | hariri chanzo]

Exester City[hariri | hariri chanzo]

Ampadu awali alicheza katika klabu ya Exeter City mwaka 2015, ambako akawa mchezaji mdogo zaidi kuonekana katika klabu hiyo ,akiwa ni mwenye umri wa miaka (15).

Chelsea F.C.[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 1 Julai 2017, Ampadu alisajiliwa kwa mkataba na klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza ya Chelsea,Akiwa na umri wa miaka 16,Hata hivyo mnamo Novemba 2017.

Mnamo 20 Septemba 2017, Ampadu alicheza mechi yake ya kwanza katika klabu hiyo ya Chelsea katika mechi mzunguko wa tatu ya EFL dhidi ya Nottingham Forest, akiingia dakika ya 55 kam mbadala wa Cesc Fàbregas.

Kufanya hivyo kukamfanya awe mchezaji wa kwanza aliyezaliwa katika miaka ya 2000 na kucheza katika timu ya Chelsea,yeye pia akawa mchezaji mdogo kabisa katika klabu hiyo kwa zaidi ya miaka kumi.Mnamo 12 Desemba 2017, alicheza Ligi Kuu akiwa na Chelsea, akiingia kama mbadala dhidi ya Huddersfield Town katika dakika ya 80.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ethan Ampadu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.