Eternal
Eternal | |
---|---|
Taarifa za awali | |
Chimbuko | London, Uingereza |
Ala | Sauti |
Miaka ya kazi | |
Studio | EMI |
Wanachama wa zamani | |
Eternal lilikuwa kundi la wasichana wa Kiingereza wanaoimba muziki wa R&B. Kundi limeanzishwa mwaka 1992 likiwa na ndugu kina Easther na Vernie Bennett, Kéllé Bryan na Louise Nurding. Kundi limepata mafanikio kimataifa, kwa kuuza nakala milioni 10 dunia nzima. Nurding ameondoka mwaka 1995 na kwenda kufanya kazi za kujitegemea kwa mafanikio tele. Bryan alivutwa mnamo 1998 na wanachama wengine wawili, ambao walidai wameondoka kwa sababu ya mahusiano kitaalamu tu. Waliobakia waliachana mwaka 2000. Walihesabiwa kama jibu la Uingereza kwa kundi la kike la Kimarekani En Vogue.[1][2]
Albamu ya kwanza ya Eternal Always & Forever (1993) ilishika nafasi ya pili kwenye chati za UK Album Chart na kwenda kupata platinamu nne huko nchini Uingereza. Mwaka wa 1997, walifika nafasi ya kwanza kwenye chati za UK Singles Chart na kibao chao cha "I Wanna Be the Only One", ambacho kiliwapatia ushindi katika tuzo za Mobo Award 1997 ikiwa kama Single Bora. Vilevile walipata kuchaguliwa mara saba kwenye tuzo za Brit Award - lakini hawajashinda. Kwa ujumla wamefanikiwa kufikia 15 hadi 20 bora nchini Uingereza kuanzia 1993 hadi 1999, huku wakiwa na 10 bora zao kwa vibao kama vile "Stay" (1993), "Oh Baby I..." (1994), "Power of a Woman" (1995), "Someday" (1996), "Secrets" (1996) na "Don't You Love Me" (1997). Mwaka wa 2013, kundi liliundwa upya wakiwa watatu bila Louise Redknapp kwa ajili ya mfululizo wa pili wa kipindi cha TV kupitia runinga ya ITV2 The Big Reunion, na kutumbuiza katika tamasha moja tu mnamo mwezi Machi 2014.[3]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Members
[hariri | hariri chanzo]Mwanachama | 1992 | 1993 | 1994 | 1995 | 1996 | 1997 | 1998 | 1999 | 2000 | 2013 | 2014 | 2015 | ||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Easther Bennett (1992–2000, 2013–hadi sasa) |
||||||||||||||
Vernie Bennett (1992–2000, 2013–hadi sasa) |
||||||||||||||
Kéllé Bryan (1992–1998, 2013–2014) |
||||||||||||||
Louise Nurding (1992–1995) |
- Tanbihi: hao walio kwenye maandishi yaliyokoozwa ni wanachama wa sasa.
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]
Albamu za studio[hariri | hariri chanzo]
|
Albamu za kompilesheni[hariri | hariri chanzo]
|
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Eternal Fansite Ilihifadhiwa 28 Machi 2012 kwenye Wayback Machine.
Book: Eternal | |
Wikipedia books are collections of articles that can be downloaded or ordered in print. |