Nenda kwa yaliyomo

Esmeralda Athanasiu-Gardeev

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Esmeralda Athanasiu-Gardeev (18341917) alikuwa mpiga kinanda na mtunzi wa muziki kutoka Romania.

Athanasiu-Gardeev alizaliwa mwaka 1834 huko Galaţi, Moldavia. Alisoma muziki mjini Bucharest na baadaye kusomea kinanda na utunzi wa muziki huko Paris chini ya Julius Schulhoff, na utunzi huko St. Petersburg chini ya Anton Rubinstein. Aliolewa na Vasile Hermaziu na baadaye na Jenerali Gardeev ambaye alimjulisha kwa tabaka la juu la warusi. Baada ya Vita ya Uhuru ya Romania, aliishi mjini Bucharest akifundisha sauti, lute, na kinanda. Alifariki mjini Bucharest mwaka 1917.[1][2]

Kazi zake zilizochaguliwa

[hariri | hariri chanzo]
  • Romanian March, Op. 1
  • Myosotis (mazurka)
  • Souvenir de Odessa (mazurka)
  • Polca capricioasa
  • Wordless romance
  • Scherzo
  • Imn (wimbo wa kwaya mchanganyiko)
  • Collection de chansons
  • 3 Leider
  1. Sadie, Stanley; Tyrrell, John (2001). The new Grove dictionary of music and musicians: Volume 2.
  2. Sadie, Julie Anne; Samuel, Rhian (1994). The Norton/Grove dictionary of women composers. ISBN 9780393034875. Iliwekwa mnamo 4 Oktoba 2010.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Ulaya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Esmeralda Athanasiu-Gardeev kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.