El Intransigente
El Intransigente | |
---|---|
Jina la gazeti | El Intransigente |
Aina ya gazeti | *. Gazeti la kila siku *. Gazeti kwenye mtandao wa tarakilishi. *. Gazeti la lugha ya Kihispania |
Lilianzishwa | 17 Aprili 1920 |
Eneo la kuchapishwa | Argentina |
Nchi | Argentina |
Mhariri | Ana Vallejo Mhariri Mkuu |
Makao Makuu ya kampuni | Buenos Aires, Argentina |
Lilikwisha | 1981 Jarida la kuchapishwa lilikwisha lakini tovuti ikaanzishwa 2008 |
Tovuti | El Intransigente |
El Intransigente lilikuwa Gazeti lililochapishwa katika mkoa wa Salta, nchini Argentina kati ya miaka ya 1920 na 1981. Shughuli zake zilianza tarehe 17 Aprili 1920 zikiendeshwa na David Michel Torino, mwanzilishi mshiriki na mmiliki wa gazeti hili. Katika miaka yake ya kwanza, El Intransigente liliunga mkono serikali ya taifa ya Hipólito Yrigoyen lakini ,hapo baadaye, likawa mwakilishi wa matakwa ya raia wengi na likatangaza masuala ya eneo hilo.
Historia yake
[hariri | hariri chanzo]Msimamo wake wa uliendelea kuwa wa kukosoa uongozi mbaya na wa kufuja mali hasa katika miaka ya 1930.Huu ukasababisha mashambulizi ya mara kwa mara. Vita yake ya kupigania uhuru wa waandishi na vyombo vya habari iliisha katika mwezi wa Juni 1981. Asili ya kufungwa kwa El Intransigente ilikuwa : kutofautiana katika mwelekeo na usimamizi wa gazeti hili hasa baada ya vifo vya wakurugenzi ,Martin and David Michel Torino. Aidha, taasisi za nchi hiyo hazikuwa imara pia wakati huo na hii ikasababisha kufungwa pia.
Miaka ishirini na saba baadaye, El intransigente likawa gazeti la kurejelewa katika tovuti kwenye mtandao wa tarakilishi. Makao makuu yake yako katika jiji la Buenos Aires.
Tovuti: El Intransigente.com
[hariri | hariri chanzo]Toleo la tovuti la gazeti la El intransigente lilianzishwa 1 Agosti 2008. Tangu wakati huo, tovuti ya gazeti hilo haijakosa wageni wanaoingia kusoma kurasa zake. Maelekezo ya uhariri yanayoamua shughuli za gazeti na kuziendesha kitaasisi yanapatikana katika kaulimbiu yake: información en estado puro (habari vile ilivyo bila kuficha)
El Intransigente.com hutoa habari ya Argentina na dunia daima kwa wasomaji wake.
Vipengele kutoka El Intransigente.com
[hariri | hariri chanzo]• Argentina (Argentina) • Mkoa (Mikoa) • Mundo (Dunia) • Sociales • Salud (Afya) • Mujer (Wasichana) • Espectáculo (Burudani) • Deportes (Michezo) • Cultura (Utamaduni) • Editoriales (Makala ya Wahariri) • Policiales • Obituarios • Turismo (Usafiri)