El Clásico

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
El Clasico mwaka 2014.

El Clásico (matamshi ya Kihispania: [el klasiko]; ya Kikatalani: El Classsic, kwa Kiingereza "The Classic") ni jina la mechi kati ya wapinzani wenye nguvu wa nchini Hispania Real Madrid FC na FC Barcelona.

Inachukuliwa kuwa moja ya mechi kubwa za soka duniani, Mechi hii inajulikana kwa kiwango chake kwa sababu huzikutanisha timu hizo bora.

Mafanikio yao[hariri | hariri chanzo]

Kwa sasa, kumbukumbu za Real Madrid na FC Barcelona kama zinalingana kwa kiasi kikubwa.

Real Madrid imeshinda: makombe 32 ya La Liga, makombe 19 ya Copa Espana, makombe 13 ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na vikombe 3 vya Intercontinental championship.

FC Barcelona imeshinda: makombe 24 ya La Liga, makombe 28 ya Copa Espana, makombe 5 ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na makombe 4 ya Intercontinental championship.

Jumla ta mechi zilizochezeka ni 271, Real Madrid imeshinda 99 na Barcelona 112, Sare 60.

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu El Clásico kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.